SHANGAZI II -4
Jina la Simulizi: SHANGAZI II
Sehemu ya : NNE (4)
Mwandishi : Aslam Khan
Ilipoishia...
"Halooo shemeji!" Ilikuwa sauti ya Monica rafiki yake Asha.
"Halooo, niambie!"
"Safi tu, kwani Asha yupo kwako?"
"Hapana, alikuwepo ila amesharudi kama masaa mawili yaliyopita!"
"Aha, sawa!"
"Kwani umeenda kuulizia kwao, hayupo?"
"Ndo nipo hapa, wamesema ameaga anatoka tangu asubuhi na atarudi kesho mchana!"
"Duh!"
"Pole shem, najua haupo peke yako katika hii dunia!" Alisema Monica na kufanya niwe na presha. Nilikataka simu kwa hasira.
Endelea...
"Vipi tena, kuna nini?" Husna aliniuliza mara baada ya kukata simu.
"Aaah hamna kitu Husna!" Niliongea huku nikimuangalia usoni.
"Wewe sema nitakusaidia!"
"Huwezi kunisaidia, kuna mtu hapa amenipigia simu anasema Asha hayupo kwao, wakati mimi alishaniambia kuwa alishafika kama masaa mawili hivi yaliyopita. Mbaya zaidi anasema anajua sipo peke yangu, najua anachokitaka huyu msichana, ananiletea maneno ili awe na mimi, nawajua hawa!"
"Aha, kumbe ndo hivyo tu, sasa wewe tatizo lako lipo wapi, mbona jambo dogo sana hilo!"
"Kivipi?"
"Mpigie simu huyo mpenzi wako yeye atakuambia yupo wapi!"
"Aha, ni sahihi!" Nilijibu huku nikiishika simu yangu na kuanza kuipiga namba ya Asha. Iliita mara ya kwanza, haikupokelewa. Ya pili haikupokelewa. Ya tatu, haikupokelewa. Ya nne haikupokelewa. Presha ilinipanda huku nikianza kuamini maneno ya Monica. Nilijaribu kupiga tena, safari hii ilikatwa.
"SAMAHANI, SUBIRI KIDOGO!" Iliingia meseji mara baada ya simu kukatwa.
"Kwani unafanya nini?" Niliituma sms, haikujibiwa.
"Asha!" Nilituma nyengine haikujibiwa. Niliamua kupiga simu. Ilikatwa. Nilipopiga tena ilikuwa haipatikani, nilifikiri labda ni matatizo ya mtandao. Nilijaribu kupiga tena lakini haikupatikana pia kuashiria haikuwa hewani.
"Vipi?" Husna aliniuliza
"Hapatikani!"
"Pole sana!" Husna alisema huku akinikumbatia. Nilihisi kufarijika sana kutokana na kile kinachonisibu. Nilijikuta nainua mikono yangu na kumshika mgongoni.
"Unajua kuna vitu vyengine unatakiwa uvijue, siku nyingi tu nilikuwa nakuonea huruma kwa sababu kuna vitu ambavyo hauvijui!"
"Vitu gani hivyo!"
"Utakuja kujua kama ukitaka!"
"Niambie, nipo tayari kujua!"
"Utakuja kujua, usijali, nikuulize?"
"Hamna shaka, niulize tu!"
"Umelifikiria ombi langu, unaweza kunipa jibu langu?"
"Husna, unanipa mtihani mzito sana!"
"Kwa nini?"
"Dah!"
"Kwani mimi sifai kuolewa na wewe!"
"Unaweza ila siwezi!"
"Sawa, ila mimi sina tatizo saana nitakusubiri mpaka siku ukitaka, hata kama miaka kumi, sio mbaya!"
"Acha uongo, miaka kumi unanisubiri mimi tu, acha kuniongopea!"
"Aaah moyo tu, kila kitu ukiamua na kujitolea kwa moyo wote, kinawezekana, nimeamua kukupenda kabisa, na sijui kwa nini moyo wangu umekuwa hivyo!"
"Hivi Husna, hauna mwanaume, manake nimejiachia tu hapa nisije nikachinjwa hapa!"
"Hakuna atakayekuchinja kwa ajili yangu, labda utachinjwa kwa sababu ya huyo demu wako, si mimi!"
"Hizo habari tuachane nazo basi!"
"Sawa, sina mwanaume mimi!"
"Na chumba na sebule anakulipia nani, na hivi vitu vyote vilivyokuwepo ndani, nani analipa?"
"Nalipia mimi mwenyewe!"
"Unafanya kazi gani, au ndo unadanga?"
"Abdam, naomba tuheshimiane!"
"Samahani sana, ila nilitaka kujua!"
"Mimi sina mambo hayo!"
"Nitaamini vipi sasa?"
"Nioe ndo utaelewa!"
"Mmmh!"
"Sikiliza Abdam, mimi nakupenda na pia mimi sio muhuni, nina kazi yangu na ndio inanifanya nijilipie hivi sehemu ya makazi na maladhi kwa ujumla, kama ukiwa tayari kunioa, utaijua kazi yangu!"
"Yaani umeniona leo tu harafu unataka nikuoe, kweli lakini?"
"Kukuona leo, sio leo tu. Kwani ni mara ngapi huwa unakuja hapa. Mimi huwa nakuona unakuja hapa na ninakuonea huruma sana, ila sikulazimishi maamuzi ni yako!"
"Una umri gani kwani?"
"Miaka ishirini na tano?"
"Miaka ishirini na tano, mwanamke harafu hauna mwanaume, kweli?"
"Ndio, sina mwanaume!"
"Umegombana nao?"
"Nimekwambia ni maamuzi tu, nilikuwa namsubiri ambaye atakuwa sahihi kwangu!"
"Kwa hiyo mimi ndo sahihi?"
"Kama ulivyosema, haujakosea!"
"Ina maana wanaume wote uliokuwa nao huko nyuma, hakuna hata mmoja uliyemuona kuwa ni mwanaume sahihi kwako?"
"Sijawahi kuwa na mwanaume tangu nizaliwe mimi?"
"Husna, acha uongo, unajua mimi sipendi uongo!"
"Najua kama hupendi uongo na ndio maana nakuambia kuwa wewe ndiye mwanaume sahihi kwangu!"
"Duh, ina maana wewe ni bikra?"
"Ndio Abdam!"
"Hahahahaha huo ndio uongo uliopitiliza hahahahah!"
"Hata sikudanganyi!"
"Hivi unafikiri nitakuamini kirahisi rahisi hivyo, unataka niingie kwenye mtego wako!"
"Abdam, nakupenda na sikudanganyi, je unataka nikuthibitishie hilo, nikuonyeshe kama sijawahi kukutana na mwanaume kimapenzi tangu nizaliwe?"