Halloween Costume ideas 2015

KAZI YA SHETANI -8

JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA         - NANE
MWANDISHI        - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com

Iliposhia…

“ Ila naomba mtambue kuwa sio kila unayemuona ana mafanikio, ana mali nyingi au maarufu sana sio kama amepatia huku mafanikio, la hasha! Wengine ni bidii ns juhudi zao ndizo zilizowafanya wafanikiwe!” alimaliza na kutufanya tujenge taswira na kuanza kuwafikiria watu maalufu wengine wakipata umaarufu kwa vitu vya kipuuzi.
“huyo kiongozi wa zamani yupo hai au ameshakufa?” niliuliza
Ýupo hai mpaka leo, uzuri wake ni kuwa ni kuwa hakuna kati ya viumbe wabaya wenye kujua pale alipo, ila kila siku wanaishi naelakini hawamjui. Kila siku wanamtafuta kwa udi na uvumba kwa kujua kuwa kuna sehemu alipojificha!” alijibu.
“wewe unamjua?” Shebby aliuliza. Yule mzee alimuangalia Shebby kwa makini kwa sekunde kadhaa.

Endelea...

“hapana, simtambui” alijibu yule mzee.
“wewe ulijuaje kama yupo hai mpaka leo na anaishi pamoja na watu wanaomtafuta?”
“nitakuja kujibu maswali yenu baadae, naomba niondoke, muda wa mkutano umeshawadia, kwa hiyo ngojeni niende kwanza!” alisema yule mzee na kuondoka. Baada ya dakika moja alirudi tena
“nilisahau, nawaomba msitoke, nitarudi muda si mrefu mkutano ukimalizika tu, mmenielewa?
“ndio!”
Tulipomjibu akaondoka katika eneo lile.
                                      *********************************************************************
Kama ilivyo ada ya kila mwezi katika nchi ya Kopsheng, kunakuwa na mkutano wa kujadili mambo mbalimbali yaliyotokea na yanayoendelea kutokea huku baadhi ya  wajumbe wakipewa nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu hali ya ufalme na utawala wake ulivyo na mapendekezo ni kwa namna gani wangependa uendeshwe ili kuleta maendeleo katika nchi yao. Hakuna hata mmoja ambaye hudiriki kusema ukweli kuhusu jinsi ambavyo wananchi wanavyoishi na vile wanavyouzungumzia utawala huo. Wengi wao husema wananchi wanafuraha na wanafurahia jinsi utawala unavyoendelea ili kuepusha kupoteza nafsi zao.miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na wajumbe ambao walikuwa wakiyapeleka moja kwa moja yale wanayoyasema wananchi juu ya utawala mbovu wa mfalme huyo. Kilichofuata kwao ni mauaji ya kikatili ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa kwa mifupa yao kwa kutumia nguvu kubwa ya maajabu na kujenga chumba maalumu kinachounganisha kiwanda cha kutengenezea jeshi la wafu na nchi ya Kopsheng. Kilikuwa ni chumba cha siri ambacho kilifahamika na baadhi tu ya washirika wa karibu wa mfalme. Tofauti na jeshi lililokuwa likifahamika na wananchi wa Kopsheng, bado alikuwa na jeshi kubwa la siri lililokuwa linaishi chini ya ardhi.
Wajumbe wengi walifurika ili kujua nini kitaongelewa na mfalme. Baada ya wajumbe na wawakilishi kuwasili katika eneo la mkutano, msaidizi wa mfalme alifungua mkutano.
“mabibi na mabwana, kama ilivyo ada yetu ya kila mwezi, tumekutana hapa ili kuweza kujadili kuhusu maendeleo na matatizo yanayoikabiri Kopsheng. Lakini mpaka muda huu bado waziri wetu hajawasili kwa hiyo tutasubiri kidogo kabla ya mkutano wetu kuanza, wakati huo mfalme wetu kuna mambo anayamalizia!” alisema mmoja wa watu wa karibu na mfalme. Baada ya dakika kadhaa, mfalme akiwa na wasaidizi wake waliwasili katika eneo la mkutano. Kwa hali ambayo haikuzoelewa, sehemu ya waziri ilikuwa tupu.
“je, kuna taarifa gani kuhusu waziri Kopsha?” aliuliza mfalme
“hatujapokea taarifa zozote kuhusu yeye mpaka sasa hivi!” alijibu mmoja wa viongozi wasaidizi wa mfalme.
“walinzi...........!”
“...ndio mfalme.....!”
“siku nyingi nina mashaka na huyu mzee, nendeni popote mutakapomkuta mukam........!” kabla mfalme hajamaliza kauli yake, waziri Kopsha aliingia katika sehemu ya mkutano hali iliyowafanya wajumbe na wawakilishi wote kusimama isipokuwa washirika wa karibu wa mfalme. Jambo hili lilikuwa likimchukiza sana mfalme. Waziri alipoketi, ndipo wajumbe na wawakilishi wananchi nao wakaketi.
 “mbona umechelewa sana kufika katika mkutano waziri na sio kawaida yako?” mfalme alimuuliza waziri Kopsha ambaye alibakia kimya tu pasi na kujibu kitu chochote.
“Kopsha, mbona umechelewa ulikuwa wapi?” aliuliza tena.
“ooooh...nilikuwa nyumbani!”
“ulikuwa unafanya nini mpaka uchelewe?”
“mimi nafikiri hawa wajumbe wote wote wapo hapa kutokana na kuambiwa kuwa kuna mkutano na sio kuhojiwa kwangu, kwa hiyo mkutano uendelee!”
“sawa ni vizuri, mkutano uendelee!” alisema mfalme akiwa amekasirika sana. Kwa siku nyingi mfalme na waziri walikuwa hawapendani kabisa. Ila mfalme alishindwa kujua ni jinsi gani ataweza kumuondoa waziri katika majukumu yake kutokana na kuwa waziri nae alikuwa na nguvu sana na karibu kila mwananchi alimpenda.
“wajumbe wote na wawakilishi wa wananchi mnaombwa usikivu ili mpate kujua ni kitu gani kilichofanya muitwe leo hii na mfalme wetu aliyetukuka!” alisema mtu wa karibu na mfalme na kuendelea
“karibu mfalme wetu mtukufu”.
Mfalme alisimama lakini hakuna mwananchi yeyote aliyempa heshima.
“kwa haraka haraka nina mambo mawili ya kuyazungumzia leo. Kabla ya yote, ndani ya ufalme wa Kopsheng tunaishi na wasaliti. Siwezi kuendelea kuona usaliti huu unatawala na kutapakaa miongoni mwa wananchi wangu. Tesh, Shen, Benjamin, Tin na Ben wote wakamatwe hapa na wauawe mbele ya macho yenu wote, ili iwe fundisho kwa yeyote atakayejaribu kusaliti ndani ya Kopsheng!”  alisema mfalme na wale aliowataja walichukuliwa na kuletwa mbele ya wajumbe.
“nikiita jina, mutampitisha mbele ili waonekane vizuri kisha mutamchinja, mmenielewa walinzi?”
“sawa!”
“Ben!” aliita mfalme na walinzi wakamchukua Ben na kuanza kumzungusha ili wajumbe wote wapate kumuona kisha akapelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya kusubiri muda wa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
“shen!” mfalme alilitaja hilo jina nae alifanyiwa kama alivyofanyiwa mwenzake na kisha kwenda kuungana na mwenzake ili kusubiri muda wao wa kunyongwa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
”Tin!”
“Benjamin!”
“Tesh!”
“huyo hayupo hapa mtukufu mfalme!” walinzi walijibu.
“kwa nini hamkumtafuta?” mfalme aliuliza kwa ukali.
“samahani mtukufu mfalme wetu, tulichelewa kupata taarifa mapema ya majina yao!”
“Tesh ni nani?”
“Tesh ni rafiki wa karibu wa Tosh, mtukufu mfalme wetu!”
“na huyo Tosh ni nani?”
“Tosh ni mtu wa karibu wa waziri Kopsha!”
“waziri Kopsha!?” mfalme aliuliza akijifanya kushangaa.
“ndio mtukufu mfalme!”
“waziri, kuna kitu gani kilichojificha hapa?”
”kujifichaje?” aliuliza waziri Kopsha.
“inawezekana wewe unaficha wahalifu!”
“kwa nini nifiche wahalifu wakati najua dawa ya wahalifu ni kitu gani!”
“unajua nini kuhusiana na Tesh?”
“hakuna chochote ninachokifahamu!”
“na kipi unachokifahamu juu ya Tosh?”
“Tosh ni mwananchi ambaye ninamtumia katika mambo yangu binafsi!”
“mambo binafsi?!, mambo gani hayo?, ya kuupindua na kuchukua kinguvu utawala wangu? Hahahahahahahah!” alisema mfalme huku akiwa anacheka kwa kejeli.
“mambo yangu hayahusiani kabisa na uhalifu wala uhaini, Tosh ninamtumia wakati nipo sehemu kama hii, yeye huwa yupo nyumbani kwangu ili kurekebisha na kuiweka nyumba katika hali ya usafi!”
“kwa hiyo Tosh kwa sasa yupo nyumbani kwako?”
Je nini kitatokea…
Usikose sehemu inayofuata.
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget