Jina la hadithi. : SHANGAZI II
Sehemu ya : KUMI (10)
Mwandishi : Aslam Khan
mawasiliano : aslammusamail@gmail.com
Ilipoishia...
Niliingia chumbani kwangu na kwa haraka niliifungua ile keki.
"NAKUPENDA SANA ABDAM!" Yalikuwa ni maneno niliyoyakuta juu ya keki. Pembeni kulikuwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe. Niliifunua na kusoma
"ABDAM, KESHO NAENDA KAZINI KUFUATILIA BAADHI YA MIPANGO YANGU. BIKRA YANGU NI MALI YAKO, HIVYO NATARAJIA KUKUPATIA KESHO KUTWA. NAKUPENDA SANA!"
Nilipomaliza kusoma moyo ulinipiga na kujikuta miguu ikifa ganzi. Macho yalinitoka mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango.
Endelea...
Nafsi yangu ilikuwa inawaza mambo mawili, nichague kupinga maamuzi ya familia yangu ili kukipata kile alichoniahidi Husna, au nikubali kwenda ili nikose kile nilichoahidiwa. Nilikuwa na mawazo mengi kiasi nilishindwa hata kuyapatia jibu la uhakika. Niliamua kumpigia simu Husna ili kumueleza hali halisi.
"Abdam...!" Sauti ya upande wa pili wa simu iliongea
"Ahsante sana Husna kwa keki!"
"Usijali!"
"Ila pia ahsante kwa ahadi uliyonipatia!"
"Oooh sawa Abdam!"
"Ila kuna tatizo limetokea!"
"Tatizo gani tena?"
"Kesho ninahitajika nisafiri!"
"Kusafiri ndio tatizo sasa?"
"Aaah yaani naenda mkoani, harafu sitarajii kurudi leo wala kesho!"
"Hilo sio tatizo!"
"Tatizo lipo!"
"Lipi?"
"Umeniahidi kesho kutwa kunipatia penzi lako, sasa huoni kama kuna tatizo hapo?"
"Ooh ndio, hilo ni tatizo sasa!"
"Nafikiria hapa nisiende, najua kama nikienda nitalikosa penzi lako, na nitakukosa milele!"
"Unataka kufanyaje?"
"Sitaki kwenda!"
"Sikiliza Abdam, usitake kugombana na wazazi wako eti kwa sababu yangu mimi, wewe nenda!"
"Sikiliza Husna, kama nikienda hiyo kesho, penzi lako nitalikosa!"
"Mimi nitakutunzia, usijali na nakuahidi utakuja kunioa wewe!"
"Aah sawa nitakuoa mie, ila tatizo mimi sitokuwa wa kwanza kupata penzi lako!"
"Wasiwasi wako ni nini mpenzi?"
"Wasiwasi wangu ni kuwa, kuna mwanaume atakuja kuwa wa kwanza kupata penzi lako kabla yangu mimi!"
"Abdam, kumbuka mimi ninajitambua, na mara nyingi sipendi kukhalifu ahadi yangu, kwa hiyo wewe usijali, kila kitu utakikuta kama vile ulivyokiacha!"
"Unataka kunidanganya tu!"
"Unafikiri nakudanganya, mara zote nakuambia jaribu kuwa mvumilivu, usipende kuwa na haraka kama hivyo!"
"Mbona uvumilivu ninao!"
"Sawa, ila hauniamini, hilo ndo tatizo lako kubwa jengine!"
"Nitakuamini vipi wakati unaniambia wewe ni bikra na sijathibitisha, pia unanificha kuhusu kazi yako!"
"Njoo basi tufanye mapenzi ili uamini ninachokuambia!"
"Sasa hivi?"
"Ndio njoo!"
"Nakuja!"
"Hebu acha utoto, jiamini mwenyewe. Lala sasa hivi, ili kesho uwahi hiyo safari yako, mimi nipo utanikuta na nakuahidi kufunga ndoa na wewe hata kama ukija kuoa mwengine!"
"Acha kunidanganya bhana!"
"Sawa kama waona nakudanganya, naomba ulale sasa hivi!"
"Sawa bhana!"
"Usiku mwema Abdam!"
"Na kwako pia!" Nilijibu nikiwa na hasira za kukosa penzi la Husna. Sikukumbuka hata kula ile keki tena, nilivuta shuka yangu na kujifunika kuanzia miguuni mpaka kichwani.
"Abdam...Abdam!" Ilikuwa ni sauti ya baba akiwa ananiamsha. Sikujua ni muda gani ulipita mpaka pale alfajiri ilipofika. Nilikuwa nimelala kwa muda mchache sana.
"Naam..!" Niliitikia nikiwa na uchovu na usingizi mwingi
"Muda huu, hebu amka ujiandae!"
"Sawa baba!" Nilijibu huku nikijilazimisha kuinuka kutoka kitandani. Niliinuka na kutoka nje mkononi nikiwa nimeshika mswaki huku kiunoni nikiwa na taulo. Nilienda nje na kusukutua kichwa na kuoga kisha nikarudi ndani. Niliposhika simu yangu ili kuangalia saa, ilikuwa yapata saa kumi na mbili kasoro. Pia kulikuwa na meseji mbili. Nilifungua ili kuzisoma.
"UNAJUA KUWA UKILIPA DENI LAKO LA TZS 1200 LEO UTAKUWA NA UWEZO WA KUKOPA ZAIDI..." Moja ilikuwa ni meseji ya deni ambalo nilikopa ili kuweka salio kwenye simu yangu. Niliifuta kabisa na kuifungua meseji nyengine.
"NAKUPENDA NA SAMAHANI KAMA NIMEKUUDHI. NIMEJITOLEA KUKUPENDA WEWE, NA NIMEKUAHIDI KUWA NITAOLEWA NAWE. KUTHIBITISHA HILO, KUNA KITU NITAKIFANYA AMBACHO KINAWEZA KUKUSHANGAZA, SIKUAMBII NI KITU GANI, BALI UTAKIONA KWA MACHO YAKO, NDANI YA MWEZI MMOJA TU." Ilikuwa ni meseji kutoka kwa Husna. Niliamua kuihifadhi. Nilivaa nguo zangu na viatu, nilipomaliza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kupaka mafuta, manukato na kuziweka nywele kwenye mtindo mzuri, nilitoka nje ya chumba changu. Nilimkuta baba akiwa sebuleni akiwa tayari amejiandaa kwa kunisindikiza kwenda kituoni. Nilitamani hii safari iwe ndoto, kwani mbali na kukosa penzi la Husna, siku kadhaa nyuma niliota ninachinjwa na mjomba mara baada ya kunifumania nikiwa ninafanya mapenzi na mkewe, shangazi. Harafu leo hii ndio ninaenda kwake kiukweli kweli. Sikuwa na jinsi, ilibidi niende tu hivyo hivyo.
"Nipo tayari!" Nilimwambia baba
"Sawa, tuondoke!" Alisema baba na kuendelea
"Chukua hii itakusaidia njiani!" Alisema huku akinipatia noti tatu za elfu kumi kumi ya kitanzania.
"Sawa, ahsante!".
Tulichukua usafiri wa kutupeleka mpaka kituoni. Tulipofika, baba alienda kukata tiketi na nikaingia ndani ya basi. Ilipofika saa moja na nusu, basi ilianza safari ya kuelekea katika mkoa wa mtwara. Watu mbalimbali walikuwa wakiwaaga ndugu na jamaa zao, kati yao alikuwa ni baba ambaye nilikuwa ninaagana nae. Nilikuwa ninaenda kwenye mkoa ambao nilikuwa siufahamu. Basi lilianza safari taratibu kutokana na foleni kubwa ya barabara ya kilwa. Kutoka mpaka kufikia mbagala rangi tatu ilituchukua nusu saa nzima. Tulipofika mbagala, basi liliingia kituoni tena, nikiwa na mawazo mengi, nilistuka mara baada ya kusikia sauti nzuri na nyororo ikiniambia jambo. Sikuelewa anaongea kitu gani, hivyo ikanibidi niinue kichwa changu ili kumuangalia aliyekuwa ananiongelesha. Alikuwa msichana, mwenye weusi wa wastani akiwa anang'aa bara bara, wenyewe wanaitaga black beauty.
"Sogea kule dirishani, hii ni siti yangu!" Alisema.
Kipi kitaendelea...
Usikose sehemu inayofuata.
Post a Comment