jina la Simulizi: SHANGAZI II
sehemu ya : KWANZA
Mwandishi: Aslam Khan
mawasiliano : 0787 378 393
: 0768 965 020
: 0627 676 104
Ilikuwa ni asubuhi, siku ambayo nilichelewa kuamka kutokana na uchovu mwingi uliipitiliza uliotokana na kazi nguvu niliyoifanya siku moja iliyopita. Nilienda nje ambapo nilipofika sebuleni, nilimkuta baba akiwa anaangalia taarifa ya habari ya saa tano katika runinga.
"habari ya asubuhi baba? " nilimsalimia
"nzuri tu, umeamkaje? "
"mimi sijambo baba, shikamoo!"
"marhaba, vipi mbona leo umechelewa kuamka sana hivyo?" baba aliniuliza
"labda ni kwa sababu ya uchovu tu, si unajua kazi zetu zenyewe za kuunga unga hizi!"
"mimi nilijua kwa sababu leo ni jumapili ndio maana ukaamua kuchelewa kuamka!"
"hapana baba, ni uchovu tu! "
"sawa, sasa hapa kuna taarifa inayokuhusu wewe!" baba aliniambia
"taarifa gani tena?"
"mjomba wako amepiga simu amesema anataka uende ukatembee!"
"mjomba gani, wa mtwara?" niliuliza
"ndio, na amesema wiki ijayo atakutumia nauli ili uende!" alisema baba huku akiniangalia.
"tooobaaaaaa!" nilijikuta neno likitoka mdomoni kwangu pasi na kutarajia
"vipi tena?" baba aliniuliza kwa mshangao
"yale yale!" nilisema
"wewe mtoto, mbona sikuelewi?"
"samahani baba, mawazo tu mengi!"
"umeshaanza kuvuta mibange sio?"
"hapana, mawazo tu, nipo mbali sana!"
"aha, kumbe mimi naongea na wewe harafu unanidharau?"
"samahani baba!"
"jiandae, wiki ijayo safari ya Mtwara!"
"sawa baba!" nilijibu huku nikiingia chumbani kwangu. Nilichukua simu na kuanza kuwasiliana na mpenzi wangu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi. Ilichukua takribani dakika kumi mpaka alipokuja kujibu ujumbe wangu, nilimuomba tuonane siku inayofuata kwa sababu nilikuwa na kitu cha kumuambia.
"mambo vipi Tom?" nilimsalimia rafiki yangu aitwae Thomas ambaye tulizoea kumuita Tom, hiyo ni baada ya kwenda sehemu anapoishi.
"safi tu, nipange!"
"dah, ebwana vipi kuhusu kesho?"
"kuhusu nini sasa?" aliuliza huku akionekana kunishangaa
"aaah hujui bwana, nazungumzia ghetto, kuna mtu aliyeweka oda(order)?"
"hahaha nilijua tu, harafu hizo tabia zenu za kuchafua mashuka harafu hata kufua hamfui, sizipendi kwanza hamlipii, munaacha maganda ya ndizi, mara michupa ya juisi, mara viepe, na wakati mwengine kondom, tunatamanishana tu, siku nyengine nitakuja tuchangie wote humu, ohooo!" Thomas alisema huku akiwa anacheka.
"hahahaha unamaanisha mtungo au? "
"wewe jichekeshe tu! "
"sasa sikiliza, mjomba bwana amepiga simu anataka wiki ijayo niende, dah sasa ndo nataka nimpange Asha, sijui atanielewa?"
"hahahh haina haja ya kumpanga wala nini, wewe ondoka sisi turithi mali, na alivyokuwa mkali, tutauana mwaka huu!" alisema huku akinipiga piga begani.
"sasa nikushangaze!"
"wewe tena, enhe, niambie!"
"usiku si nimeota nachinjwa mwenzio, harafu sababu kubwa ni kutembea na shangazi, mjomba alitufuma tunafanya mapenzi sebuleni, na yeye akaungana na sisi. Mimi si ndo nikaona kumbe mjomba amependa, hivyo nikajiamini, heeee kumbe ana lake bwana, ile najifuta baada ya kumaliza nastukia nimepigwa kichwani harafu nikazimia. Sijakaa sawa mara nachinjwa, hatari sana!"
"harafu unaamka unaambiwa uende huko huko ulikoota unachinjwa?"
"eti! "
"hahah ingekuwa mimi wala nisingeenda!"
"mimi sasa sina cha kufanya!"
"kwanza nenda, ukitangulia, tutamuhudumia shemeji, hahaha hainaga ushemeji tunakulaaaaa.... Hainaga ushemeji tunakulaaaaagaaaaaa, na mimi napitaaaa uhuuuuu!" alisema Thomas huku akicheza cheza.
"nitakuua!"
"haha wewe uliona wapi maiti inaua, hebu tuachane na hayo, unakuja saa ngapi?"
"sijajua bado, ingekuwa mimi ndiye niliyekuwa na maamuzi, basi hata asubuhi, ila si unajua mtoto wa kike mambo mengi sana, hiyo ndo shida!"
"sawa, wewe asubuhi njoo uchukue funguo, ila zingatia usafi bwana!"
"usijali kaka!"
"okay!"
"sasa ngoja mimi niende nyumbani, nitakucheki jioni, manake mzee yupo leo, inabidi nikae karibu karibu, si unajua fuata nyuki ule asali! "
"hamna shida!"
Nilimuaga Thomas na kurudi nyumbani.
***
Siku ya pili niliamka saa moja na kuishika simu yangu. Nilimpigia Asha ili nijue atakuja saa ngapu.
"halooooo!" ilisikika sauti upande wa pili, alikuwa asha.
"umeamkaje?"
"sijambo sijui wewe?"
"nimeamka salama, vipi utakuja saa ngapi?"
"hata sijajua bado!"
"hujajua, acha utoto wewe!"
"aaah jamani, basi nitakuja saa sita!"
"Njoo saa nne!"
"heeeeh saa nne?"
"ndio!"
"chai je?"
"tatizo lako nini, wewe njoo nitajua mimi!"
"na nikija unanipeleka wapi?"
"nyumbani! "
"akhaaaa, nyumbani kwenu naogopa mie!"
"basi wewe usijali, njoo nitajua mimi, sawa!"
"sawa, ila nyumbani kwenu sitaki....!"
"sawa, ila na wewe usichelewe kuja!"
"sawa!"
Nilikata simu na kutoka nje kwa ajili ya kunywa chai. Nilipomaliza kunywa, nilienda mpaka kwa Thomas ili kuchukua funguo za chumba chake ambacho ningekitumia kwa siku hiyo. Nilipofika pale, sikumkuta, chumba kilikuwa kimefungwa. Nilimfuata mpangaji mmoja ili nimuulize kuhusu Thomas.
"habari yako dada?"
"nzuri tu, mzima wewe?"
"mimi mzima, vipi huyu Tom, ameenda wapi?"
"sijajua, nimemuona tu anatoka asubuhi, ila sijajua kama kaenda wapi!"
"dah!" nilisema huku nikishika kidevu changu
"vipi tena Abdam?" yule dada aliniuliza hali iliyonifanya nishangae
"heeh unanijua?" nilimuuliza
"ndio, kwani vibaya?"
"hapana, je una namba zake?"
"ndio, ngoja nikupe!" alisema yule dada na kuingia ndani kisha akarudi na simu yake. Alinitajia namba kisha nikaziingiza kwenye simu yangu na kumpigia Thomas. Simu iliita bila ya kupokelewa. Baadae iliita nikaambiwa inatumika.
"sahamani, simu unayopiga haipatikani mwaka huu!" yalikuwa ni maneno niliyoyasikia baada ya kuendelea kupiga simu kwa muda mrefu.
"dah, ina maana ameamua kunizimia simu, dah!" wakati nasikitika, simu yang iliingia meseji, nikajua labda Tom atakuwa amenitumia
"baby, mie ndo nipo kwenye gari hapa, tunakaribia kufika"
"dah!" nilizidi kuchanganyikiwa mara baada ya kupokea meseji hiyo.
"pole sana kaka angu, abdam, najua kinachokutatiza, ila mie nilimsikia Tom akisema tangu jana kuwa anataka kuwakomesha, ila usijali!" alisema yule dada huku akinishika begani.
"mmmmh!" niliguna
"mimi nitakusaidia, ila kwa masharti!"
Je ni masharti gani hayo?
Usikose sehemu inayofuata kwa majibu ya swali hili.
Toa ushauri na maoni yako.
ANGALIZO- Yule uliyenae ndiye atakufanya uwe na kibamia au tango, usiongeze maumbile ni hatari kwa afya yako.
Post a Comment