Jina la hadithi. : SHANGAZI II
Sehemu ya : KUMI NA MBILI (12)
Mwandishi : Aslam Khan
mawasiliano : +255 (0) 627 676 104
aslamstorymail@gmail.com
aslamstory.wordpress.com
Ilipoishia...
"Hamna kitu, unataka tuwe tunachat?"
"Wewe tu, sio mbaya!"
"Sawa!" Nilijibu huku nikifikiria neno la kuanza nalo. Nilitafakari kwa muda, mara simu yangu ikatoa sauti tena.
"NIAMBIE, MBONA KIMYA!" Meseji kutoka kwa Tunda ilisomeka.
"TUNDA...!"
"ABEE!"
"WEWE NI MZURI SANA!" Nilimtumia meseji iliyomfanya Tunda kuguna.
"Wewe!" Nilisikia maneno yakiwa yamemtoka Tunda. Nilianza kuwa na wasi wasi.
"HIVI NIKUULIZE?" Tunda alinitumia meseji hiyo
Endelea nayo…
“NIULIZE TU TUNDA” nilimjibu kwa njia ile ile ya meseji
“AAH AU BASI” Tunda alinitumia meseji.
“NIULIZE TU JAMANI!” nilimtumia meseji kwa shauku ya kutaka kufahamu alitaka kuniuliza kuhusu kitu gani.
“BASI SUBIRI, NITAKUULIZA TUKITOKA KULA, SI UNAJUA TUMESHAFIKA NANGURUKULU” Tuna alinitumia meseji
“SAWA!” sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali tu kile alichoiniambia.
Tulikaa kwa takribani dakika kumi na tano pasi na mtu yeyote umsemesha mwenzake mpaka tulipofika katika mji wa NANGURUKULU m ji ambao kwa magari yote ya abiria yaendayo katika mikoa ya kusini mwa Tanzania huweka kituo cha muda ili kuwapa nafasi abiria wao kupata chakula.
“vipi hauendi kula?” Tunda aliniuliza
“nitaenda labda kujisaidia tu” nilisema huku nikiipigia mahesabu kiasi kidogo cha pesa kije kunisaidia katika siku zinazofuata.
“kujisaidia kila mmoja ataenda, nazungumzia kwenda kula chakula” Tunda alisisitiza
“huo ni mtihani sasa!” nilisema
“kivipi”
“yaani hapo ni sawa na kwenda kujisaidia pale unapokwenda kujisaidia wewe!” nilisema.
“kwani kwenda kujisaidia pale ninapokwenda kujisaidia mimi ni vibaya?” Tunda aliniuliza.
“sio vibaya, ila inakuwa ni suala lisilowezekana!”
“hakuna kisichowezekana, na mie nimeshakuelewa kuwa hutaki kwenda kula kwa sababu hauna hela, twende tu, mie nitakununulia ukitakacho!” Tunda alisema kwa kujiamini.
“mmmmmh…..!” niliishia kuguna tu. Niliongozana na Tunda mpaka kwenye mlango wa choo ambapo niliingia kwenye choo cha kiume na yeye kuingia katika choo cha wanawake. Baada ya muda mfupi kila mmoja alirudi akiwa ameshakidhi haja yake. Kilichofuata ni kwenda sehemu ambayo vyakula huuzwa. Ilitubidi kuchukua vyakula kwenye sehemu maalumu ili kwenda kula ndani ya basi kutokana na muda kuwa mdogo sana. Mimi sikuwa na ubavu wa kuagiza chakula change kutokana na chakula chenyewe ninanunuliwa, hivyo niliona hata aibu. Tunda aliagiza niwekewe chipsi kavu pamoja na kuku nusu. Tulifungasha vyakula vyetu mpaka ndani ya gari na kuanza kula taratibu huku stori za uongo na kweli zikiwa zinasindikiza mlo wetu. Muda mchache tangu tulipoanza kula, gari lilianza kuondoka katika eneo la Nangurukulu na kushika njia inayoelekea Kilwa kilanjelanje mpaka somanga. Kwa stori tulizokuwa tunaongea, ungetukuta, ungeweza kusema kuwa tulikuwa tunafahamiana kwa kipindi kirefu.baada ya kumaliza kula, kila mmoja alijisafisha kwa tishu na kunywa maji ya kutosha. Hapo nilihisi usingizi ukiwa unaninyemelea kwa mbali. Nilijitahidi nisilale.
“Tunda, kwani bado sana kufika?” nilimuuliza mara baada ya kupita muda mrefu wa safari.
“dah, bado, ndo kwanza tupo Mandawa hapa!” alijibu Tunda
“basi mie nalala kidogo, utaniamsha basi” nilimwambia Tunda.
“mimi mwenyewe nalala, ila nafikiri nitawahi kuamka kabla yako”
“sawa Tunda uniamshe, nisije nikapitishwa!” nilisema
“unaposhuka ndio mwisho wa gari, utapitishwa vipi sasa hahahahaha” alijibu Tunda huku akicheka.
“aaah mie sijui sasa na wewe wanicheka”
“hahahah tulale bhana!” alijibu tunda na kila mmoja akajiweka katika mkao mzuri wa kuutafuta usingizi. Baada ya muda mchache kila mmoja alilala. Sikujua nililala kwa muda gani, ila nilistuka ninaamshwa na Tunda huku mkono wangu ukiwa ndani ya blauzi aliyokuwa ameivaa Tunda. Ulikuwa katika eneo la tumbo lake. Nilistuka sana na kuutoa mkono wangu haraka haraka. Nilimtazama Tunda kwa aibu, nikitamani kumuomba msamaha lakini kutokana na aibu iliyonijaa, nilishindwa kabisa. Haraka haraka niliishika simu yangu na kugeukia dirishani kisha nikaingia upande wa kuandika ujumbe mfupi wa maandishi. Nilitafuta namba ya Tunda.
“SAMAHANI SANA TUNDA!” nilituma ujumbe kwa Tunda huku nikiwa ninasikilizia majibu kutoka kwa Tunda. Baada ya muda simu ya Tunda ilitoa mlio. Aliichukua na kuiangalia kisha akaniangalia na kutabasamu.
“ABDAM, UNA MPENZI KWANI?” ndio lililokuwa jibu la Tunda.
“KWA NINI WANIULIZA HIVYO?” nilijibu swali kwa swali badala ya swali kwa jibu.
“KWANI HILI NDO JIBU LAKE?” aliuliza. Nilikaa kwa muda nikitafakari nimpe jibu gani. Niliona hakukuwa na haja ya kumdanganya, bora kumwambia ukweli tu.
“NDIO NINAYE!” nilijibu kwa kifupi
”ANAITWA NANI?” aliuliza
“HUSNA!” nilizidi kujibu kwa kifupi
“ANAKAA WAPI?” alizidi kuuliza maswali.
“YUPO DAR ES SALAAM!”
“SAWA!” alijibu kwa kifupi. Baada ya hapo tulikaa kimya kwa dakika nyingi pasi na mtu kumsemesha mwenzake
“Tunda…!” nilivunja ukimya
“niambie Abdam…!”
“hapa tulipo muda huu ni wapi, maana nimetumiwa ujumbe sasa nashindwa kuwajibu!”
“ahaa hapa tupo Mchinga, muda si mrefu sana tutaingia katika mkoa wa Lindi”
“aha, sawa ahsante sana!”
“swala hili tu ndo likufanye ushukuru, mbona kuna mengi nyuma hata shukrani haujatoa?”
“aaaah jamani Tunda, samahani sana jamani!”
“achana na hayo, nakutania tu!”
“sawa bhana”
“si unaona hapa, hapa zamani kabla ya barabara kujengwa, huu mlima ntunaoenda kuupanda sasa hivi, ulikuwa na mtindo wa herufi S, basi ajali kila siku zilikuwa zinatokea!” Tunda alisema.
“inaonyesha ni kwa kiasi gani ulivyokuwa mwenyeji….!” Nilitania
“sio sana, maana najua tu historia chache chache za milima ya huku. Tangu zamani mlima huu wa mamba, mlima wa kikwetu au mamburu kwa jina jengine, mlima wa mbanja, mmongo, na ule wa mingoyo ndio iliyokuwa milima ya hatari, achilia ile milima kama unaenda masasi kama nanyamba huko newala!”
“mmmmh mbona kama umeanza kunidanganya tena?”
“hahahah tuachane na hayo Abdam!” alisema Tunda na kunishika katika paja.
“Tunda….!” Niliita.
“ niambie Abdam…!”
“aaah uliponishika, sio mahali sahihi…!” nilisema.
“aaah jamani, hapa tu, mbona maajabu tena!”
“unaona kawaida au, nikikushika wewe utakubali?”
“kwenye paja tu, mbona ni kawaida tu…!”
“kawaida eeeeh, si ndio?”
“ndio….!” Aliitikia Tunda. Niliona anajifanya kichwa maji, niliamua kumkomesha.
“kwa hiyo na mimi nikikushika ni kawaida tu, sio” nilimuuliza kwa kumtega.
“aah ndio…!”
Aliponijibu, nilipeleka mkono wangu mpaka kwenye sketi yake juu ya paja lake. Niliweka mkono wangu juu yake, na taratibu nikaanza kutomasa kutomasa.
“mmmmmmmmmh…..!” nilisikia anaanza kuguna.
“vipi tena Tunda!”
“kwa hiyo umeamua kunikomoa, sio?”
“kwa nini?” nilimuuliza kwa kejeli.
“samahani, naomba uniache!” alisema kwa sauti ndogo naya chini iliyokuwa legevu sana
“basi siku nyengine ukiwa unaambiwa, uwe unasikiliza!”
“usijali Abdam, ila ongera sana”
“ongera ya nini Tunda?”
“subiri nitakuambia… kwa sasa acha kwanza niwasiliane na wenyeji wangu!” alisema Tunda na kushika simu yake. Kuanzia hapo hatukuongea tena mpaka tulipofika katika mkoa wa Mtwara, katika kituo cha gari za abilia. Tulipofika, hata nafasi ya kuagana hatukuipata, kwa sababu muda wote alikuwa yupo bize kweli kweli. Nilishuka kwenye basin a kupokelewa na mjomba. Kila muda nilikuwa naangalia angalia nyuma labda ningeweza kumuona Tunda, lakini sikumuona kabisa.
“mjomba vipi tena, kuna mtu umekuja nae nini?” mjomba aliniuliza alipoona kila muda nikiwa ninaangalia angalia nyuma.
“hahahahahah hamna mjomba, naangalia angalia tu mji wenu huu!” nilisema.
“sawa, sasa sisi tunakaa NKANALEDI na ndiko tutakapoenda ila baada siku chache zijazo, tutahamia Sabasaba au Chikongola, umenielewa mjomba?”
“aha, sawa!” nilijibu huku niinua simu yangu na kuiangalia.
“aaaah kumbe simu nilitoa mlio, angalia meseji tatu na simu mbili nilizozikosa” nilisema na kuanza kuzifungua meseji.
“VIPI MPENZI, UMEFIKA SALAMA, NAONA NAKUPIGIA SIMU HAUPOKEI, NATAKA NIKWAMBIE KUWA NAWEKA MAMBO YANGU VIZURI NA KARIBUNI NITAKUJA HUKO, SIWEZI KUISHI PEKE YANGU ABDAM, SIWEZI KABISA, NAKUPENDA SANA!” Ilikuwa meseji kutoka kwa Husna. Nilipanga nitaenda kuiijibu pindi nitakapokuwa nimetulia kwa mjomba. Niliifungua meseji ya pili.
“EBWANA ABDAM, ASHA ALITAKA KUJINYONGA, HIVYO AMELAZWA HOSPITALI, HAJITAMBUI!” ilikuwa meseji kutoka kwa Thomas ama Tom kama tulivyozoea kumuita. Yeye sikutaka kabisa kumjibu meseji yake na mpenzi wake, Asha.
“ANGALIA MBELE ABDAM USIJE UKAMWAGA BIASHARA ZA WATU, NAJUA UNANITAFUTA, MIMI NAKUONA. HUWEZI KUNIONA MAANA NIPO NDANI YA GARI LENYE VIOO VYEUSI. UKWELI NINA HISIA NAWE, NA NITAKUTAFUTA……!” Meseji ya mwisho ilikuwa inatoka kwa Tunda.
Je kipi kitatokea na Tunda?, na je vipi kuhusu Husna kama akisafiri itakuaje na je nini hatma ya Asha?
Usikose sehemu inayofuata.
Post a Comment