Halloween Costume ideas 2015

KAZI YA SHETANI -6

JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA         - SITA
MWANDISHI        - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com

Iliposhia…

“wale ni wapelelezi na wale waliokuwa na rangi nyeusi na kijivu askari kwa ajili ya mauaji. Inavyoonekana taarifa za kuja kwenu hapa zimeshajulikana. Wale wana uwezo wa kujua wanaomtafuta yupo wapi au ameelekea wapi. Pale wameshindwa kujua upande mlioelekea kwa sababu ya hiyo fimbo. Hiyo fimbo ni msaada mkubwa kama itatumika ipasavyo. Hiyo sio fimbo kama munavyoiona. Hiyo ni dagger maalumu yenye uwezo wa kuua mashetani ya kijini na kibinadamu pia. Wote walioshindikana kutokana na uhalifu wao, hapo ndio mwisho wao. Inafanya kazi kutokana na fikra za mtu aliyeichukua. Ina uwezo wa kubadilika na kuwa silaha yeyote kulingana na matumizi ya wakati husika” alisema.
“Dagger ndio nini?” shebby aliuliza 

Endelea…
“dagger ni lugha tu ya kigeni, maana yake ni visu vidogo vyenye ncha kali vinavyotumika katika mapambano ya karibu au close combat kwa lugha nyengine. Ila kwa huku kwetu dagger ni visu maalumu vilivyonakshiwa na kupambwa na lugha za kijini. Mara nyingi vilitumika katika kuwaangamiza viumbe ambao sio wa kawaida. Visu hivi vilikuwa vinatumika miaka mingi iliyopita katika falme ya uajemi katika dunia yenu na chimbuko lake ni huku. Vilitolewa kwa ajili ya kuleta amani miongoni mwa falme ingawa wengine walikuja kutumia vibaya na kusababisha machafuko ambayo yanaendelea mpaka leo. Tofauti na visu vyengine, visu hivi huwa na rangi ya dhahabu na vito viwili katika mpini wake. Upande mmoja huwa na kito cha rangi ya kijani na upande wa pili kito cha rangi nyekundu” alisema. Wakati huo bado tulikuwa tukimfuata yule mzee kwa njia ya mstaari. Nilijaribu kuiangalia vizuri ile fimbo na ndani ya zile nakshi, ulionekana kitu mithili ya kimiminika cha rangi ya dhahabu ambacho kilikuwa kinatembea tembea. Wakati nikiendelea kuangalia kwa makini, nilistuka baada ya ile fimbo kujichora herufi “A” na baadae kujichora maandishi ambayo nilikuwa siyafahamu. Niliogopa sana.
“mzee, angalia hii ni nini sasa?” nilimuuliza huku nikimuonyesha ile fimbo. Mzee alikataa kuishika ile fimbo.
“inaonekana una bahati sana!” alisema na kuendelea
“kuanzia leo hiyo fimbo utakuwa nayo siku zote za maisha yako. Hiyo inaonyesha kuwa wewe utakuja kupata matatizo sana hapo baadae, kwa hiyo fimbo imekuchagua wewe kuambatana nayo mpaka pale matatizo yatakapokwisha” alisema.
“mbona sielewi mimi?” nilimuambia.
“utakuja kuelewa tu, kuna kitu unamfanyia mjomba wako kwa hiyo lazima kuna jambo baya litakuja kukutokea , pia naona una mpenzi huku huku!” alisema huku akiendelea kucheka.
“.....ila tuyaache hayo, la umuhimu ni kuwasaidia kuweza kurudi duniani salama..!” alisema.kila mmoja alishangaa juu ya matukio yaliyokuwa yakiendelea huku.
“karibuni nyumbani kwangu, tumeshafika!” alisema baada ya kutumia dakika thelathini na saba tangu pale tulipokutana nae mpaka kufika pale alipokuwa anasema ni nyumbani kwake.
“nyumbani kwako?” tulimuuliza huku tukistaajabu kwa sababu hakukuwa na dalili zozote za uwepo wa makazi ya watu katika maeneo hayo, bado kulikuwa kunaonekana kuwepo kwa jangwa tu.
“ndio, hapa ndipo ninapokaa” alijibu huku akituamuru tumsubirie tumsubirie oale mpaka atakaporudi.
“hamruhusiwi kusogea hata hatua moja!” alisema huku akianza kuondoka. Tulimuangalia akiwa anatembea kwa takribani mita saba tokea pale alipotuacha kisha akapotea. Hali ile ilitufanya tustuke sana mpaka Tina akakimbia toka pale tulipokuwa tumekaa. Sekunde mbili tu tangu alipokimbia,ghafla alianguka chini. Pale pale aliumia vibaya kwenye mguu. Tulimchukua na kwenda nae pale alipotuacha yule mzee.
“ndo umefanya nini tena Tina?” aliuliza Hamza. Lakini Tina hakuwa na jibu badala yake alikuwa akiugulia maumivu.
“hampaswi kuogopa, lazima tushikamane na kuwa majasiri!” alisema Shebby.
“kweli kabisa, kwa sababu hata tukisema tukimbie, tutakimbilia wapi, huku kote hakuna hata mmoja kati yetu mwenye kupajua hapa!” alichangia Aziza.
“ni kweli, unaweza kkukimbia hapa harafu ukaenda kukamatwa na watu wa kiongozi wao. Itakuwa umefanya nini sasa, kama huyu mzee angekuwa ni mtu mbaya wala tusingefanikiwa kufika kufikia katika eneo hili angetuacha tuangamizwe na wale viumbe!” nilisema
“swadakta!” alichangia Hamza na Aziza.
Tulikaa pale tukimsubiria yule mzee. Baadae alikuja akiwa ameshika chupa ndogo ndogo tano kulingana na idadi yetu zenye maji maji ya rangi ya zambarau. Alitugawia kila mmoja chupa moja na kutuamuru tunywe akisema ni dawa ya kujitambua.
“mtakapokunywa hii dawa, wale wenye kuwafuatilia hawatoweza tena kujua mahali mlipo hivyo kutawafanya kuwa salama zaidi mpaka pale suala la kurudi kwenu duniani litakapokamilika!” alisema kwa msisitizo
Hakukuwa na majadiliano zaidi kuhusu suala  la kunywa zile dawa. Kila mmoja alitaka abaki akiwa salama kabisa npaka pale suala la kusaidiwa kurudi duniani litakapokamilika. Kila mmoja alichukua chupa yake na kuanza kuinywa. Mara baada ya kunywa ile dawa, taratibu nguvu zilianza kuniishiana baadae nuru ilianza kupotea machoni kwangu. Baadae ilitoweka kabisa na kujikuta sijitambui. Sijui ni kwa muda gani nililala pale chini, ila baadae nilikuja kuzinduka na kukuta mazingira yamebadilika sana. Niliwaangalia wenzangu, Aziza alikuwa tayari ameshaamka kabla yangu. Hamza na Tina ndo walikuwa wanaanza kuzinduka kutoka katika ule usingizi. Baada ya dakika moja, Shebby nae akaamka. Nilipoangaza vizuri pembeni, ile fimbo sikuiona, badala yake kulikuwa na kisu chenye urefu wa sentimita kama ishirini hivi. Kilikuwa kimenakshiwa na dhahabu tupu katika mpini huku kukiwa na maandishi ambayo sikuweza kuelewa yalikuwa ni ya lugha gani. Pia katika mpini kulikuwa na kitu chenye umbo la duara chenye kung’aa sana. Upande mmoja kilikuwa cha rangi ya kijani na upande mwengine kilikuwa cha rangi nyekundu. Kwenye makali yake, kulikuwa na maandishi yaliyokuwa yanatoa nuru ya ajabu. Niliinuka toka pale chini na kuangaza huku na huko. Kulikuwa na miti michache, nyumba na nyasi lakini vyote vilikuwa na rangi moja tu, nyeupe. Nilijaribu kuangalia juu, hakukuwa na mawingu wala jua wala mwezi. Mwanga wa kawaida tu ambao chanzo chake sikupata kukifahamu ndio uliokuwepo katika eneo hili. Yule mzee alikuja pale tulipokuwa tumekaa.
“habari zenu!” alitusalimia.
“salama!”
“nyie mnalala sana!” alisema
“ni kwa kipindi gani tulikuwa tumelala?” Hamza aliuliza.
“ni wiki mbili sasa!”
“aaah, wiki mbili tupo hapa hapa tu, hahahaha hilo haliwezekani kabisa!” alisema Shebby.
“ndo hivyo wiki mbili, mlikuwa mmelala haha nje, nilikuwa nawageuza geuza tu hapa kama samaki wanaokaangwa!”
“duh, sasa si tungekufa kwa njaa, siku zote hizo!” nilisema.
“kikubwa sasa hivi, karibuni ndani!” alisema na kuanza kuondoka pale, tulimfuata.
Yule mzee alipita nyuma ya nyumba yake ambako kulikuwa na bustani ya kuvutia. Tulifika katika bustani hii na kukaa hapo. Nyumba ya huyu mzee ilikuwa ya kawaida sana, kwa muonekano wa nje. Tukiwa pale bustanini, Yule mzee aliingia ndani na kurudi na matunda ambayo nilikuwa ninayafahamu kabisa. Kulikuwa na matufaha, makongomanga, mapeasi, mananasi na matunda mengine mengi. Kilikuwa kilichosheheni matunda mengi sana.
“kuleni haya matunda!” alisema Yule mzee mara baada ya kutuletea kile kikapu.
“wewe je, hauli?” tulimuuliza.
“muda wa kula bado, kwa mwezi tunakula mara moja tu!”
Itaendelea…
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget