Halloween Costume ideas 2015

KAZI YA SHETANI -4

JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA         - NNE
MWANDISHI        - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com

Iliposhia…

“haujui?, hebu elezea ilikuwaje ukawa katika sehemu hii, yaani tukio la mwasho kulikumbuka?”
“ahnha ni..ni...nili...nilikuwa natoka nyumbani ili kuelekea kwa rafiki yangu ghafla nikiwa njiani nikahisi kuishiwa nguvu harafu kuna upepo nikahisi ulikukwa unavuma sana. Ulikuwa ni upepo mkali sana hali iliyonifanya kufumba macho ili mchanga usije ukaingia machoni. Nilishindwa kukimbia kutokana na kuishiwa nguvu. Baada ya dakika kadhaa nguvu zilirudi na ule upepo ulikuwa umeisha. Nilipokuja kufungua macho, nilistaajabu kwa sababu sikuwepo pale, nilikuwa katika sehemu nyengine, sehemu yenye mazingira ambayo siyafahamu, ni mazingira haya katika sehemu hii!” alimaliza hamza. Ilikuwa ni hadithi ya kustaajabisha kidogo.

Endelea…

“oooooh! Kumbe, enhe na wewe unaitwa nani?” aliuliza tena yule mzee.
“Tina!”
“Tina, unapajua huko ulikotoka?”
“hapana sipajui”
“enhe na hapa ulipo unapafahamu?”
“hapana!”
“na wewe ilikuwaje ukawa katika eneo hili ambalo haulifahamu?”
“nikiwa natoka kwa shangazi ambako niliagizwa na mama, ilibidi nivuke barabara ili nipate kurejea nyumbani. Niliangalia kulia na kushoto bila ya kuona gari yeyote inayokuja. Nikiwa katikati ya barabara, ghafla nilijikuta nimerushwa juu nikadondoka chini. Pale pale watu walijaa na niliwasikia tu wakisema tumpeleke hospitali, mara wengine wakisema nimeshaaga dunia tayari. Taratibu nuru ilipotea machoni kwangu na baadae nikalala kabisa. Nilipokuja kuamka ndio nikajikuta nipo katika eneo hili.”
“mh! Na wewe unaitwa  nani?”
“Aziza!”
“ilikuaje ukawa katika sehemu ambayo hauifahamu?”
“mimi?”
“Ndio wewe, au unapajua hapa?”
“hapana!”
“enhe ilikuwaje sasa?”
Aziza nae akaeleza jinsi ambavyo alifika pale.
“Sawa!” alisema yule mzee mara baada ya Aziza kumaliza kuhadithia njia illiyomfanya kufika pale.
“wewe unaitwa nani?” aliuliza yule mzee huku akiniangalia mimi. Sikujibu kitu bali nikageukia pembeni tu.
“nakuuliza wewe hapo!” alisema yule mzee huku akinishika begani.
“sijajua ni imani kiasi gani niliyonayo kwako mpaka nikutajie jina langu, kama sipati msaada mpaka nikutajie jina langu, basi” nilijibu lakini nikiwa na woga sana.
“hakuna kitu chenye kufichika huku, hauwezi kunificha kitu kabisa, wewe unaitwa nani?”alisema yule mzee na kuonyeshea kidole mwanaume mwengine.
“shebby!”
“Shebby?”
“ndio!”
“na wewe kwako ilikuwaje ukafika hapa, au unapajua hapa?”
“ndio napajua!” alijibu Shebby hali iliyofanya wote tustuke na kubaki tukishangaa kile alichokijibu Shebby. Ina maana muda wote tuliokuwa tunasumbuka kutafuta msaada, kumbe shebby alikuwa anapafahamu huku tulipo.
Tuliona huyu anaweza kuwa ni mtu mbaya kwetu. Uaminifu juu yake ukapotea.
                                   *************************************************************
Ni katika makao makuu ya Kopsheng, mfalme alionekana katika chumba chake cha siri akiwa na baadhi ya wasaidizi wake muhimu.
“nipeni taarifa, ni kitu gani kinachoendelea kusikika miongoni mwa wananchi wangu?” aliuliza mfalme.
“mtukufu mfalme, kutokana na tetesi zinazoongelewa na walio miongoni mwa wananchi wako ni kuhusu suala la utawala wako. Ila kubwa na lililonistua ni tetesi za kuupindua utawala wako, hilo ndilo kubwa na hayo ndio yaliyonifikia kutoka kwa wapelelezi wetu walio katika kila kona ya ufalme wako. Alijibu mmoja wa washirika.
“sawa, kazi nzuri Eldon, kwa hiyo hawa wananchi bado wana mipango ya kuupindua ufalme wangu kweli, nawashangaa tu, hawa ni viumbe gani wasiokata tamaa, kila atakayejaribu nitampeleka kule anakostahiki, kuzimu!” alisema mfalme.
“kitu kingine ninachohisi ni kuwa, nyuma ya hawa wananchi wapo viongozi ambao muda wote tupo nao muda wote katika shughuli zote za kifalme” alisema Eldon.
“Eldon, kwa kutumia uwezo wako mkubwa wa miujiza ulionao, bado tu haujapata kuwajua hao walio nyuma ya wananchi ambao wana mpango wa kuubomoa ufalme wangu?” aliuliza mfalme.
“hapana kiongozi, inaonekana hao walio nyuma ya wananchi wana uwezo mkubwa sana kuliko ule niliokuwa nao mimi!” alisema Eldon.
“hebu subiri kwanza niangalie huyo fukunyuku ni akina nani!” alisema mfalme na kufumba macho yakehuku akiwa ameibana miguu yake kwa nguvu kama mtu anayeizuia haja ndogo isitoke. Ilimchukua dakika tatu kuwa katika hali hiyo. Alifumbua macho na kisha kuwaangalia wasaidizi wake mmoja baada ya mwengine.
“wapo waasi kumi na moja, ila kuna watano nimeshindwa kuwatambua. Niliowatambua ni Tesh, Shen, Wesh, Tin, benjamini na Intiswari, sasa hawa munajua ni kitu gani cha kufanya juu yao. Sasa ili kuweza kuwatambua wengine ambao nimeshindwa kuwatambua, nipeni majina ya wapiganaji wenye uwezo mkubwa ndani ya ufalme wa Kopsheng wanaoitwa mashujaa. Nafikiri hao ndio wanaweza kuwa miongoni mwa hawa watano ambao sijawafahamu” alisema mfalme.
“aaah mtukufu mfalme wangu, hao ni waziri Kopsha, kuna mtu wake wa karibu anaitwa Tosh, mwanawe waziri Kopsha anayeitwa Tush, wengine ni Angel, Samson, mfalme aliyepita anayeitwa Cysery pamoja na mmoja hivi ambaye sifahamu jina lake halisi ila jina la utani anaitwa Black bird. Pia kuna wengine kama wanne hivi majina yao siyafahamu mtukufu mfalme” alisema Eldon
“kuanzia sasa amuru wapelelezi wetu kuwafuatilia kwa ukaribu zaidi hao wasaliti, hasa Kopsha, umenielewa Edmund, na Eldon atakuwa ndiye kiongozi wao” alisema mfalme.
“ndio mtukufu wangu, hilo halina shida, ila Invy amesema ana taarifa ambayo itakuwa ni ya kustusha sana, kwa heshima yako namuomba atoe hiyo taarifa” alisema Edmund Jackson huku akimuangalia mfalme ambaye alitoa ruhusa kwa ishara ya kunyoosha mkono.
“mtukufu mfalme, kupitia kwa wapelelezi ninaowaongoza mimi, tumegundua uwepo wa binadamu ambao wamekuja kwa njia isiyo  rasmi, kutokana na ratiba niliyoipata toka kwa anayeratibu safari na mialiko yote tunayowapatia, amesema hakuna ratiba yeyote ya safari ya binadamu yeyote aliyepangiwa kuja huku kwa muda huu” alisema Invy.
“usiwe na shaka sana juu ya suala hilo Invy. Mmoja kati ya hao watu ni mtumishi wetu anayeitwa Alfonse  Daniel, nafikiri wengi wenu munamtambua. Kwa hiyo yeye atatuletea taarifa zote kama ujio wa watu hao ni wa kheri au ni wa shari.
“lakini mtukufu, kutokana na taarifa za awali zinasema kuwa watu hao hakuna hata mmoja aliyekuwa amedhamiria kuja huku.sasa hapa ndio kwenye mkanganyiko, kama hawajapanga huku kuna mambo mawili, la kwanza wamekuja kwa bahati mbaya labda walitolewa kafara ila haijakamilika ndo wamekuwa ni wazururaji huku, au pili inawezekana kuna mmoja wa wananchi amewaleta huku, ila kwa nini waletwe wakati huu, hapo ndipo wasi wasi wangu unapoongezeka!” alisema Edmund kwa msisitizo
“wewe taarifa za kuwa watu hao wamekuja hapa pasi na kukusudia umezipata wapi? Aliuliza mfalme.
“kiongozi umesahau kuwa mimi ndiye msaidizi wako?, taarifa juu ya ujio wa hao binadamu nilipozipata toka kwa Alfonse Daniel tu, nilifanya uchunguzi na kuyagundua hayo. Ni jukumu langu kuhakikisha himaya yako inakuwa salama siku zote mtukufu mfalme wangu!” alisema Edmund.
“sawa vizuri sana” alisema mfalme huku akimpigapiga Edmund begani.
“tusipoangalia hapa, tutashindwa vibaya sana kwa siku zijazo, hilo ni kutokana na kushindwa kupatikana kwa kito chenye rangi ya bluu kilichopo katika kisiwa kimoja katika dunia” alisema mfalme
“nimekuelewa kiogozi wangu mtukufu!”alijibu Edmund.
“je kuna taarifa nyengine ya ziada?” aliulliza mfalme
“ndio kiongozi, kuna Magreth Kimario na Lawrence Majoka walitaka kuja huku ili kukamilisha kafara zao juu ya mahitaji yao kama walivyoahidi, wanasubiria ruhusa yako tu” alisema Eldon.
“Edmund taarifa hizi ni za kweli?” mfalme aliuliza.

Je taarifa hizo ni za kweli au uongo, usikose sehemu inayofuata
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget