Halloween Costume ideas 2015

SHANGAZI II -5


 Jina la Simulizi: SHANGAZI II

Sehemu  ya       : TANO (5)

Mwandishi        : Aslam Khan



Ilipoishia...


"Duh, ina maana wewe ni bikra?"

"Ndio Abdam!"

"Hahahahaha huo ndio uongo uliopitiliza hahahahah!"

"Hata sikudanganyi!"

"Hivi unafikiri nitakuamini kirahisi rahisi hivyo, unataka niingie kwenye mtego wako!"

"Abdam, nakupenda na sikudanganyi, je unataka nikuthibitishie hilo, nikuonyeshe kama sijawahi kukutana na mwanaume kimapenzi tangu nizaliwe?"


Endelea...


"Achana na hayo, harafu unajua unanishangaza Husna, basi tu!" Nilimwambia

"Kitu gani kinachokufanya unishangae hivyo?"

"Unatoa wapi ujasiri wa kuniambia maneno yote hayo?"

"Abdam, ujasiri ni asili ya mtu, mimi ni mtu mzima, najielewa na sijui kitu gani ambacho ni kigeni sana nilichokifanya mimi?"

"Tena unaongea bila ya aibu kwangu, mmmh!"

"Aibu, zama hizo zilishapitwa na wakati, kama utaishi kama hivyo si unaweza ukajikuta kitu ambacho kilikuwa chako unakikosa hivi hivi, mambo hayo ni ya kizamani. Mtu ukimpenda unamwambia, akikataa ndo changamoto zenyewe, tatizo liko wapi?"

"Aah sawa!"

"Nakusikiliza!"

"Husna, samahani sana, sipo sawa mwenzako!"

"Jambo gani hasa tofauti na hili linalokufanya uwe kwenye hali hiyo!"

"Unaona hili ni jambo dogo eeeh?"

"Abdam, unatakiwa kuwa shupavu, utakuja kujisababishia matatizo kutokana na mambo kama hayo!"

"Matatizo, matatizo yapo tu, lazima mtu utetee kitu chako!"

"Basi mimi nakuomba uende ukapumzike kwenu, ila simu usizime kwani nina kitu cha kukuonyesha ambacho haukijui!"

"Sasa si uniambie tu!"

"Hapana, wewe nenda kapumzike kwanza!" Alisema Husna huku akiniangalia kwa huruma.

Ilikuwa ni takribani majira ya saa kumi na mbili hivi, nilitoka chumbani kwa Husna na kuanza kuongoza kwenda nyumbani. Nilipofika nyumbani, hata hamu ya kula sikuwa nayo, nikaenda moja kwa moja kitandani. Lakini kutokana na joto kali la Dar es salaam, ilinilazimu kwenda kuoga, hivyo sikupinga. Nilienda kujimwagia maji na kurudi chumbani kwangu!

"Abdam, chakula tayari!" Mama aliniita 

"Najisikia kama kushiba shiba hivi!"

"Mbona haujasema kama tusikujumuishe pamoja, sasa harafu nimeshapakua, njoo ule!" Alisema mama hali iliyonifanya nisiweze kupinga kauli yake. Nilitoka chumbani kwangu na kwenda sebuleni, sehemu iliyokuwa imeandaliwa chakula. 

"Jiandae andae bwana, wiki inayo tu, uende ukasafishe macho!" Alisema baba.

"Sawa, ila nako si mjini tu kama huku?"

"Mji kila sehemu upo, usiwe na shaka kabisa!"

"Na ukienda huko, ukatulie hukoo!" Alisema mama

"Hilo halina shida sana kwangu!" Nilijibu kwa kujiamini. Tuliendelea kula huku tukiwa tunaongea hili na lile. Tulipomaliza, ndugu yangu aliondoa vyombo na mimi nikaingia chumbani kwangu huku nikiwa nawaza kuhusu tukio lililotokea mchana. Niliamua kumpigia simu Thomas ili nimlaumu kwa kumkejeli kwa kitu alichonifanyia lakini nikifanikiwa kutumia chumba cha Husna. Nilipiga simu, haikupokelewa kwa mara ya kwanza. Nilipiga tena, ndipo ilipopokelewa.

"Halooo!"

"Mambo Tom!"

"Safi tu, niambie!" Aliongea kwa sauti iliyokuwa inasikika ikiwa imejaa uchovu au usingizi, sauti ya kivivu.

"Freshi, naona leo umeamua kunikomoa, sio?"

"Kukukomoa kivipi mdau?"

"Tumekubaliana vizuri, harafu umenifanyia nini sasa?"

"Kukufanyia kitu gani?"

"Dah, jamaa yangu si tumekubaliana nije kuchukua funguo harafu umenitosa hivi hivi!"

"Kwani chumba chako au changu?"

"Dah, cha kwako bro!"

"Basi poa, nimechoka muda huu, acha nipumzike na mama watoto hapa!"

"Aha, kumbe ukiwa na demu ndo unanijibu jeuli hata mimi, nitakuja kumtimua huyo!" Nilitania

"Njoo ufe kwa presha...!"

"Kwa nini unasema hivyo?"

"Umenikatishia mechi bwana, na mechi ya leo ni kali kweli kweli, wewe nitafute kesho, ila chumba changu sitaki, nataka kuoa!"

"Mmmmmmm....h!"

"Yah, ujumbe umefika!"

"Duh...!"

"Ndo hivyo!"

"Mmmhh....oooooohh... Baby.... Achan....naaa... Na ....mpuuzi huyooooo.... Nata....kaaaa....yote...... Siku....baniiiiiiiiiiiiiiiii!" Nilisikia sauti ya mwanamke akilalamika kimahaba kutokana na raha ya tendo la ndoa.

"Duh, mimi ndo mpuuzi?"

"Tena zaidi ya ulivyosikia, siku moja utakuja kujua kwa nini wewe ni mpuuzi!" Alijibu Thomas na kukata simu. Nilifikiria sana maneno ya Thomas yalikuwa yanamaanisha nini, lakini sikuwa na jibu. Niliamua kumpigia simu Husna, kwa sababu mara nyingi huwa alikuwa ananiliwaza ninapokuwa na mawazo.

"Husna!"

"Niambie Abdam!"

"Dah, mwenzio hapa sipati usingizi kabisa!"

"Lazima usipate, ila wakati mwengine inabidi ukubaliane na ukweli halisi ili uishi vizuri!"

"Sasa nampigia simu Thomas, alichonijibu na kunifanyia, sijaamini kabisa yaani!"

"Sikia, adui mara nyingi hujifananisha na wewe ili usimjue!"

"Kwa nini unasema hayo?"

"Njoo sasa hivi, nataka kulala nawe kuna baridi sana eti!"

"Acha utani bwana, unajua niko serious?"

"Najua, basi njoo mara moja kuna kitu unatakiwa kukijua!" 

"Kwa nini usiniambie tu!"

"Wewe si uje bwana, unajua mimi nakusaidia wewe, harafu naona unazingua zingua!"

"Dah, usijali, nakuja!" Nilimjibu, huku nikiinuka toka kitandani. Ilikuwa yapata saa tano hivi za usiku. Nilivaa nguo zangu na kutoka nje, kuelekea kwa Husna. Nilipofika niligonga mlango wa chumba anachoishi Husna. 

"Ooh umefika?" Alisema Husna mara baada ya kutoka nje.

"Mbona unauliza jibu, hapo bado kuchukua rula na kupigia mstari tu ulionyooka!"

"Sawa, sasa nenda katika dirisha la rafiki yako ukasikilize!"

"Usinichoshe bwana, nimepita anafanya mapenzi, sasa nikasikilize nini?"

"Inaonyesha haujagundua kitu, nenda harafu mimi naenda kumgongea!"

"Sawa!" Nilijibu huku nikienda karibu na dirisha na kukaa nikisikiliza sauti zinazosikika tokea ndani. Sauti zile zilikuwa zinaniumiza kwa kiasi kikubwa. Mara mlango wa chumba cha Tom uligongwa.

"Dah!" Tom alilalamika.

"Nani tena huyo?" Yule msichana aliuliza. Sauti yake nilikuwa kama naifaham. Tom alitoka nje na kwenda kuongea na Husna ambaye alijifanya kuulizia namba zangu za simu huku Tom akisema hana namba zangu.

"Ulikuwa unaongea na nani?" Sauti ya mwanamke ilisikika ndani ya chumba cha Tom.

"Anataka namba za Abdam, ni jirani hapa!"

"Jirani ndo mwanamke, usiku huu, huyo ni demu wako!" Alilalamika, na kuifanya sauti yake isikike vizuri!"

"Ashaaaaaaaa!!!??????!!!!!...." Nilijikuta nikiropoka kwa sauti kubwa.

"Aaaaaaaah!" Sauti mbili kutoka katika chumba cha Thomas zilisikika zikishangaa kutokana na kusikika kwa sauti yangu.


Je nini kitatokea...... Usikose sehemu inayofuata.

Itaendelea

!

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget