Halloween Costume ideas 2015

KAZI YA SHETANI -7

JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA         - SABA
MWANDISHI        - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com

Iliposhia…

Yule mzee alipita nyuma ya nyumba yake ambako kulikuwa na bustani ya kuvutia. Tulifika katika bustani hii na kukaa hapo. Nyumba ya huyu mzee ilikuwa ya kawaida sana, kwa muonekano wa nje. Tukiwa pale bustanini, Yule mzee aliingia ndani na kurudi na matunda ambayo nilikuwa ninayafahamu kabisa. Kulikuwa na matufaha, makongomanga, mapeasi, mananasi na matunda mengine mengi. Kilikuwa kilichosheheni matunda mengi sana.
“kuleni haya matunda!” alisema Yule mzee mara baada ya kutuletea kile kikapu.
“wewe je, hauli?” tulimuuliza.
“muda wa kula bado, kwa mwezi tunakula mara moja tu!”

Endelea…

“heeee, mwezi! Si mtakufa kwa njaa?” aliuliza Shebby.
“huko duniani kwenu ni tofauti na huku.na mimi ni tofauti na wewe!” alijibu.
“haya mazingira, hakuna jua, hakuna mwezi hizo siku mnazihesabu vipi?” aliuliza Aziza.
“mimi ni mkazi wa huku pia kumbuka kuwa mimi sio binadamu kama unavyoniona wewe. Pia nina uwezo wa kufanya jambo linaloweza kukushangaza wewe, mfano angalia hii.....!” alisema Yule mzee huku akichukua tufaha moja ambalo baadae lilioza na funza walianza kutoka katika lile tunda. Baadae alichukua wale funza na kuwaweka mkononi kish kuwatupa chini na wakageuka kuwa mkate.
“vipi unaweza kula huu mkate?” aliuliza
“ aaaaaah wewe hapana!” tulijibu huku tukijizuia kutapika.
“kuna mwenye swali?” aliuliza.
“ndio!” alijibu Aziza.
“enhe!”
“mzee itachukua muda gani mpaka pale tutakapopata msaada wa kurudi nyumbani salama?”
“jambo zuri kwa muda huu ni kuhakikisha kuwa munakuwa salama kwa kipindi chote mtakachokuwa mpo huku. Kuhusu suala la lini au kwa kipindi gani mtafanikiwa kurudi ni juhudi na kujitambua kwenu tu!” alijibu.
“kujitambua na juhudi kivipi, hatujakuelewa babu!” Shebby aliuliza.
“kujitambua na juhudi, yaani pale mtakapokuwa tayari kurejea kwenu tu, mtarejea!”
“sisi tupo tayari!”
“ndio mpo tayari ila hamjajitambua kama mpo tayari na wala hakuna juhudi mlizozionyesha kuhusu kuwa tayari”
“dah, mzee hatujaelewa kabisa!”
“usijali, bado siku kadhaa tu mtakuja kuelewa!” alisema yule mzee na kuendelea
“kuna swali jengine?”
“ndio, mimi hapa ninalo!” nilijibu
“uliza!”
“mimi nina maswali kama manne hivi!”
“sawa, uliza moja moja!” alisema.
“hili ni eneo gani?”
“ni eneo tunaloishi sisi!”
“mwanzo ulisema kuwa, watu maalumu ndio wanaopaswa kuja huku, ni wepi hao hatu maalumu?”  niliuliza.
“watu maalumu ni binadamu ambao wanajulikana sana kwa maarufu walio nao utokanao na kile wanachokifanya kama msanii, mfanya kazi, mfanya biashara na kadhalika!”
“na mualiko maalumu ni mualiko wa aina gani?”
“unaonekana mdadisi sana wewe, mambo mmengine yatakuletea matatizo matatizo sana hapo baadae, ila sawa mwaliko maalumu ni mualiko ambao aina binadamu niliokutajia huupata mara baada ya kuuomba na kusubiria majibu yao kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja!”
“swali langu la misho, pia ulisema kazi maalumu, je kazi maalumu ifanyikayo huku ni kazi gani?”
“kama ningejua kuwa maswali yako yanahusiana na vitu hivyo ulivyoniuliza, ningekuambia uniulize yote kwa mara moja” alisema na kumeza funda moja la mate na kuendelea
“Jambo ninalotaka mufahamu kwanza ni kuwa dunia yenu ina watu wachache wema ila wengi wao ni watu wabaya. Miaka kadhaa iliyopita eneo hili lilikuwa ni eneo ambalo lilikuwa likitoa msaada katika sayari mbalimbali ikiwemo na dunia yenu. Kama mtakumbuka au sijui kama mlishawahi kusikia kama matukio ya ajabu ajabu yanayotokea katika dunia yenu katika siku za hivi karibuni kama zamani yalikuwepo. Kwa siku za hivi karibuni, nguvu  zitokazo katika eneo hili zinatumika kwa njia isiyofaa. Hasa ni baada ya kiongozi huyu anayeongoza kwa sasa kuchukua madaraka kwa nguvu kutoka kwa mfalme ambaye alikuwa hapendelei upuuzi kama huu unaoendelea. Siku hizi eneo hili limekuwa ni eneo la kumwaga damu za viumbe wasio na hatia tu. Watu wengi huja huku kwa tamaa ya kupata mali, umaarufu au kupandishwa cheo kazini. Kwa mfano, anakuja anayejiita mwanasayansi anapewa vimelea vya ugonjwa ambao duniani kwenu haupo, kwa kutumia wadudu na wanyama kama nzi, mbu au hata popo ama mbwa wanaeneza ugonjwa huo kwa binadamu. Wanaacha kwanza uue watu kadhaa ndipo hujitokeza na kusema wanafanya uchunguzi juu ya kupata dawa ama chanjo yake kumbe tayari dawa yake wanakuwa wanayo tangu kabla ugonjwa haujaenezwa. Baadae huisambaza dawa na kupata fedha nyingi, kutokan na kutokujua kwenu munawapongeza na kuwaona wameokoa maisha ya binadamu kumbe munawapongeza wauaji. Sasa kazi maalumu ambayo huja kufanywa huku na hao watu ni kuwatoa sadaka binadamu wenzao kama malipo ya kile wanachopatia. Mfano kama mtu anamiliki magari hasa ya abiria, huja huku kwa huyu mfalme na kuchagua ni gari gani anataka kafara ya damu itoke. Ndipo unapoona gari limepata ajali harafu watu wamefariki. Huku kuna viumbe ambao wamepangiwa kazi yao ni kusababisha ajali tu. Hao wana uwezo wa kumfanya dereva asinzie wakati anaendesha kwa mwendo wa kasi au kumfanya mtu anywe pombe kupita kiasi harafu akaendesha chombo cha moto. Wengine kazi yao ni kuwatoa viumbe nakala. Pale ajali inapotokea huja huyo kiumbe ambaye humtoa mtu nakala, yaani huwa watu wawili waliofanana kila kitu. Baada ya hapo huja wengine ambao kazi yao kubwa ni kuwachukua wale waliokuwa watu haswa ambao kiukweli huwa wameumia kidogo na kuondoka nao, huwa hawajafa kwa sababu mungu pekee ndiye mwenye amri ya kuchukua roho ya kiumbe wake. Zile nakala huachwa katika eneo la ajali na pindi wanapokuja madaktari husema wale watu wamefariki. Inabidi lazima zile nakala zife kwa sababu kwa sababu mtu mmoja hatakiwi kuishi kwenye nafsi mbili tofauti. Wale watu wakishaletwa huku hutolewa kiasi kidogo cha damu na kasha hutumikishwa kwa hiyo kazi maalumu wanayokuja kuifanya huku ni kupata mali, umaarufu, na pia kutoa sadaka ya binadamu. Ila naomba mtambue kuwa sio kila unayemuona ana mafanikio, ana mali nyingi au maarufu sana sio kama amepatia huku mafanikio, la hasha! Wengine ni bidii na juhudi zao ndizo zilizowafanya wafanikiwe!” alimaliza na kutufanya tujenge taswira na kuanza kuwafikiria watu maalufu wengine wakipata umaarufu kwa vitu vya kipuuzi.
“huyo kiongozi wa zamani yupo hai au ameshakufa?” niliuliza
Ýupo hai mpaka leo, uzuri wake ni kuwa ni kuwa hakuna kati ya viumbe wabaya wenye kujua pale alipo, ila kila siku wanaishi naelakini hawamjui. Kila siku wanamtafuta kwa udi na uvumba kwa kujua kuwa kuna sehemu alipojificha!” alijibu.
“wewe unamjua?” Shebby aliuliza. Yule mzee alimuangalia Shebby kwa makini kwa sekunde kadhaa.

Je atajibu nini, usikose sehemu inayofuata.

Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget