Halloween Costume ideas 2015

SHANGAZI II -6


 Jina la Simulizi: SHANGAZI II

Sehemu  ya       : SITA (6)

Mwandishi        : Aslam Khan


Ilipoishia...


"Nani tena huyo?" Yule msichana aliuliza. Sauti yake nilikuwa kama naifaham. Tom alitoka nje na kwenda kuongea na Husna ambaye alijifanya kuulizia namba zangu za simu huku Tom akisema hana namba zangu.

"Ulikuwa unaongea na nani?" Sauti ya mwanamke ilisikika ndani ya chumba cha Tom.

"Anataka namba za Abdam, ni jirani hapa!"

"Jirani ndo mwanamke, usiku huu, huyo ni demu wako!" Alilalamika, na kuifanya sauti yake isikike vizuri!"

"Ashaaaaaaaa!!!??????!!!!!...." Nilijikuta nikiropoka kwa sauti kubwa.

"Aaaaaaaah!" Sauti mbili kutoka katika chumba cha Thomas zilisikika zikishangaa kutokana na kusikika kwa sauti yangu.


Endelea...


Nguvu ziliniishia. Kichwa changu kilitawaliwa na mawazo lukuki juu ya uamuzi ambao ningeufanya sekunde chache zijazo. Niliwaza nikachukue kisu niwachome wote, mara akili nyengine ikanijia nijinyonge. Nilijitahidi kufikicha macho yangu ili niamke kwenye hii ndoto inayonitesa, lakini haikuwa ndoto. Niliwaza cha kufanya kwa muda kisha niliamua kwenda ndani, kwenda chumbani kwa Thomas kwa ajili ya kuanzisha vurugu na kutetea mali yangu. 

"Abdam, unaenda kufanya nini tena!" Husna aliniuliza mara baada ya kuniona nikiwa na hasira nikielekea chumbani kwa Thomas swali ambalo halikupata jibu tokea kwangu.

"We Abdam....!" Alisema Husna huku akinikimbilia na kunishika nisiende kule aliko Thomas. Nguvu zake zilikuwa ni ndogo sana kwa wakati ule. Nilimsukuma, lakini alining'ang'ania kwa kunikumbatia mgongoni.

"Husna, niache...!" Nilisema huku nikijaribu kumtoa asinishike.

"Abdam, hapana, usifanye hivyo!" 

"Husna, niache tafadhali!" Nilisema huku nikiwa nimekaribia kabisa kufikia katika chumba cha Thomas. 

"Achana nae bwana, wanawake si wapo wengi, utajaza watu hapa harafu itakuletea picha mbaya!"

"Husna, husna, husna tafadhali!"

"Nakuomba, nipo chini ya miguu yako, usigombane nao nakuomba Abdam, nitakupa chochote unachokitaka ila sio kugombana nao!"

"Poa, sigombani nao, niache niende!"

"Unanihakikishia hilo?"

"Ndio Husna, sigombani na mtu!"

Husna aliniacha kwa kuamini kuwa nisingeenda kuanzisha ugomvi.

"Funguo mlango!" Nilisema mara baada ya kufika mlangoni kwa Thomas

"Tumelala bwana, usitusumbue!" thomas alijibu

"Tom, fungua mlango, fungua mlangoo!" Nikisema huku nikiupiga piga mlango.

"Mbona kelele nyingi?" Tom aliuliza.

"Wewe si mwanaume, unaogopa nini kufungua mlango, si unajiamini wewe, fungua mlango tuongee kama wanaume!"

"Usifikiri nakuogopa au sijiamini!"

"Fungua sasa!" Nilisema kwa hasira.

"Ngoja, nakuja!" Alijibu Thomas kwa kujiamini na baada ya dakika kadhaa alifungua mlango!

"Haya unasemaje!"

"Shida yangu ni huyu malaya, na sio wewe!" Nilisema na kuingia ndani kwa nguvu na kumfanya Thomas kuanguka sakafuni.

"Weeeee ole wako umguse huyo!" Alisema Thomas lakini alikuwa ameshachelewa, kwani tayari nilishafika pale alipo Asha na kumchapa kibao kimoja kitakatifu kilichomdondosha mpaka kitandani.

"Kwa nini unanifanyia hivi Asha!" Niliuliza swali ambalo Asha hakunijibu badala yake alikuwa analia tu.

"Kwa nini, nakuuliza wewe kwa nini lakini?"

"Sikupendiiiiiiiiii.......!" Alisema Asha kwa sauti kubwa hali iliyonifanya mwili wote kuingiwa na ganzi na kujikuta bila ya kutegemea nikimpiga makofi mawili. Nilikuwa natetemeka kwa hasira. Nilijuta kwa nini nilikuja kushuhudia tukio kama hili, tukio linaloumiza moyo. 

"Unasemaje?" Niliuliza bila ya kushangaa kilichokuwa kimesikika.

"Sikupendi, sikupendi Abdam...tokaaaaaaa!" Alirudia tena Asha

"Wewe...we...." Nilisema kwa hasira iliyojawa na kigugumizi huku nikimsogelea ili nikampe kofi jengine.

"Tulia rafiki yangu!" Alisema Thomas huku akinishika

"Niacheee, sina urafiki na wewe...!" Nilisema huku nikiuondoa mkono wake kwangu

"Wewe mwanaume bwana, msikilize anachosema, amesema hakupendi, ya nini kutaka kuanzisha ugomvi tena, hebu fikiria kwani ulimkuta bikra huyu, hiyo inamaanisha wapo walioanza kupita. Nasikitika kukuambia kuwa kabla ya kwako, mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kabisa, na bikra yake ilikuwa ni mali yangu kwa maana nilimtoa mimi bikra. Unajua wapi, mimi ni mtu wa kigoma, na huyu Asha ni wa huko huko. Kijiji chetu kinaitwa mgambazi na huko ndiko tulipokuwa wapenzi. Kwa bahati mbaya yeye alitangulia kuja huku ila tulikuwa tunawasiliana kila siku. Nisifu tu mimi rafiki yako kwa kuvumilia sana na kuwa mpole pale ulipokuwa unalala nae kwenye kitanda changu. Sasa kwa bahati mbaya leo uvumilivu umenishinda na ndio maana nikaamua kutokuachia funguo za chumba changu. Kaka hii ni mali yangu, pole sana kwa maumivu. Najua inaumiza sana, ila lazima uukubali ukweli kuwa Asha sio mali yako, ni mali ya Tom, au Thomas. Wewe tafuta mwengine, na kuanzia leo sitaki kuona unampigia simu Asha, wala kuniomba chumba kwa ajili kulala na demu wako. Kinachonisikitisha zaidi, ulijifanya hutaki kuwa na mwanamke mwengine kwa kuamini kuwa Asha ni wako peke yako, hapo ulifeli, nakukumbusha kuwa siku zote lazima uwe na spea bwana, kama gari tairi zake mnabeba na spea, sembuse kwa demu, hasa kwa hawa wa karne hii wasioaminika, shauri yako utaumia sana tu, naomba uondoke sasa hivi chumbani kwangu tunataka tulale. Kwa leo nakusamehe kwa kumpiga mke wangu mtarajiwa, ila ikitokea siku nyengine, utanijua mimi ni nani!" Alimaliza Thomas na kunionyesha kuwa natakiwa kutoka chumbani kwake. Nguvu zilizidi kuniishia. Nilihisi nataka kudondoka. Miguu ilikuwa inatetemeka na kunifanya nishindwe kutembea. Machozi yalikuwa yananibubujika bila ya sauti ya kulia kutoka. Kamasi nazo hazikuwa mbali, zilikuwa kila muda zinachungulia chungulia. 

"Abdam, tuondoke!" Alisema Husna na kunishika mkono ili tuondoke. Nilishindwa kutembea.

"Abdam, mimi nipo, nakuahidi nitakufanyia kila kitu, nakupenda!" Alisema mbele ya Asha na Thomas. Asha alishangaa sana kusikia vile. Kiumbo na kisura, Husna alikuwa anavutia zaidi ya Asha. Pia alikuwa ana akili sana za kimaisha tofauti na Asha mwenye akili za kitoto kitoto.

"Abdam, twende bwana!" Alizidi kuongea Husna lakini macho yangu bado yalibakia kwa Asha. Husna alipoona hivyo, alisimama mbele yangu na kusogeza midomo yake kwenye midomo yangu kisha kuuingiza ulimi wake katika kinywa changu na kuuzungusha katika ulimi wangu. Hali ile iliufanya moyo wangu kupoa na uume wangu ulianza kusimama. Nikainua mikono yangu na kukishika kiuno cha Husna ambaye alivaa dela wenyewe wanaita kijola, na chupi tu ndani. 

"Abdam...!" Ilisikika sauti ya Asha ambaye alikuwa anainuka kutoka kitandani kuja nilipokuwa nimesimama na Husna.


Je kipi kitatokea? Usikose sehemu inayofuata


Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget