Halloween Costume ideas 2015

KAZI YA SHETANI -9

JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA         - TISA
MWANDISHI        - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com

Iliposhia…

“inawezekana wewe unaficha wahalifu!”
“kwa nini nifiche wahalifu wakati najua dawa ya wahalifu ni kitu gani!”
“unajua nini kuhusiana na Tesh?”
“hakuna chochote ninachokifahamu!”
“na kipi unachokifahamu juu ya Tosh?”
“Tosh ni mwananchi ambaye ninamtumia katika mambo yangu binafsi!”
“mambo binafsi?!, mambo gani hayo?, ya kuupindua na kuchukua kinguvu utawala wangu? Hahahahahahahah!” alisema mfalme huku akiwa anacheka kwa kejeli.
“mambo yangu hayahusiani kabisa na uhalifu wala uhaini, Tosh ninamtumia wakati nipo sehemu kama hii, yeye huwa yupo nyumbani kwangu ili kurekebisha na kuiweka nyumba katika hali ya usafi!”
“kwa hiyo Tosh kwa sasa yupo nyumbani kwako?” 

Endelea…

“hayupo!”
“yupo wapi?”
“sipajui pale alipo!”
“acha upuuzi, wewe unaficha wahalifu nyumbani kwako!” mfalme alisema kwa kuhamaki huku akinyanyuka kutoka katika kiti chake cha kifalme.
Taratibu maumbile ya mfalme yalianza kubadilika na kuwa kiumbe wa ajabu. Hali hii iliwafanya wajumbe waliokuwepo pale kuanza kuingiwa na woga. Alianza kuwa na umbile kubwa na taratibu kucha za miguu na mikono zilianza kuchomoka na kuwa ndefu. Meno nayo yalikuwa kama ya kiumbe anayekula nyama. Masikio yalikuwa marefu kama fey na mbawa zilianza kumtoka. Waziri Kopsha alivyoona vile, nae akaanza kubadilika ili kuwa tayari kujitetea kwa kile kitakachotokea. Waziri alikuwa nyoka mkubwa sana mwenye pembe mbili kichwani na miguu sita. Wakati mfalme akiwa anamwelekea waziri Kopsha, mmoja wa wasaidizi wake alienda na kumnong’oneza jambo hali iliyomfanya mfalme kubadilika kurudi katika hali yake ya kawaida na akarudi kukaa pale katika kiti cha enzi cha kifalme huku akiwa amejawa na hasira. Waziri Kopsha nae alirudi katika umbile la kawaida na kwenda katika sehemu yake na kukaa.
“wajumbe tunaomba radhi kwa kile kilichotokea hapa ila tunapenda kuwataarifu kuwa mkutano umeisha kwa leo. Pindi mutakapohitajika tena mtataarifiwa” alisema msaidizi wa mfalme na kisha mfalme na wasaidizi wake wakaondoka. Kwa kile kilichotokea, hakuna hata mmoja aliyekumbuka kuhusu watu waliotakiwa kuuliwa kwa makosa yausaliti. Wajumbe na washirka wote walindoka katika eneo la mkutano huku kila mmoja akiwa na jambo la kusimulia katika familia zao.
                                                     ********************************
Tulikaa pale mara baada ya yule mzee kuondoka kuelekea katika mkutano. Tuliangalia angalia katika eneo lile ambalo lilikuwa ni eneo zuri sana. Tulianza kuzunguka zunguka ili kuangalia na kufurahia uzuri wa eneo lile la bustani. Ukubwa wa bustani hii, ulikuwa sawa na ukubwa wa kiwanja cha mpira wa miguu au zaidi yake. Nilipokuwa naendelea kuzunguka katika ile bustani, nilimuona Aziza akiwa katika eneo lenye vipepeo wengi sana. Alikuwa amekaa chini akionekana kufurahia upepo mwanana wa sehemu hii. Niliamua kumfuata ili kuongea nae mambo kadhaa.
“vipi Aziza?”
“poa, niambie!”
“naona unakamata vipepeo hapa?!”
“yeah!, unapenda na wewe kucheza na vipepeo?”
“aaah, mimi sio mtoto kama wewe!”
“hahahahaa kwa hiyo mimi ni mtoto, sio?
“kwani haujioni kama wewe ni mtoto kuliko mimi?”
“una ukubwa gani wewe mwanaume?” alisema Aziza huku akiinuka na kusimama kisha kuniangalia usoni.
“wewe ni mtoto kabisa kwangu!”
“sema tu    unataka ubishi wewe!”
“sio ubishi, una miaka mingapi?”
“kumi na minane!”
“sasa si nilikuambia wewe ni mdogo kabisa kwangu?”
“kwani wewe una miaka mingapi?”
“ishirini na tatu!”
“kwa hiyo miaka ishirini na tatu tu, unajiona mkubwa sana eeeh?”
“kwani hauoni ni miaka mingapi niliyokupita?”
“mitano!”
“sasa je, waonaje?”
“hauna ukubwa huo hata kidogo!”
“unaniweza mimi?”
“kukuweza kivipi?”
“nakuuliza mimi ni saizi yako?”
“hata ungekuwa na miaka ishirini na nane, bado ungekuwa ni saizi yangu tu!”
“kivipi?”
“hivyo hivyo unavyomaanisha wewe!”
“kama……!”
“vyovyote vile unavyofikiria!” alisema Aziza wakati tukiwa tunatembea tembea katika bustani. Tulienda katika sehemu ambayo kilikuwa na maporomoko ya maji. Tulitafuta sehemu moja iliyo nzuri ili tuketi. Tulikaa juu ya jiwe moja huku tukiangalia maji yaliyokuwa takitiririka Taratibu. Ajabu katika maporomoko haya, yalikuwa ni maji yaliyokuwa kama mvua tu kwa sababu hakukuwa na mlima ingawa maji haya yalikkuwa yakidondoka kama katika maporomoko mlimani. Ilikuwa ni eneo linalovutia sana.
“kuwaza kama vipi?” nilimuuliza
“kwani wewe unawaza nini?”
“unanipenda?”
“ndio nakupenda!”
“kweli?”
 “kwanza unamaanisha kivipi?”
“wewe unanipendaje kwani?”
“kibinadamu, kama watu ambao tupo katika matatizo pamoja, tupendane ili tupate msaada pamoja!”
“anha kumbe?”
“ndio hivyo, au wewe una kitu za ziada unataka kuniambia?”
“hapana!”
“kweli?”
“waangalie hao wanaokuja huku!” nilimwambia Aziza huku nikimuonyesha ujio wa Shebby na Tina.
“aaaah wapendanao hao!” alisema Shebby.
“nawaona hapo!” nilisema
“naona hapo mpaka kitaeleweka tu, muda wote huo mliokaa hapa?” alitania Shebby.
“aah wapi, hanipendi huyu!” nilisema huku nikimuangalia Aziza
“mmmh ndivyo nilivyokuambia?” aliuliza Aziza kwa sauti ya chini, sikumjibu.
“munaenda wapi huku?” niliwauliza
“tumesikia bwana, mjibu mwenzako huko!” alisema Tina.
“nitamjibu!” nilisema.
“hahahahahahaha anaona aibu mwanaume mzima, hebu tuondoke Tina tuwaache kama kweli atamjibu!” alisema Shebby huku akimshika mkono Tina na kuondoka katika eneo tulilokuwa tumekaa.
“enhe, niambie!” nilimwambia Aziza mara baada ya Shebby na Tina kuondoka katika eneo lile.
“nikuambie kitu gani?”
“wewe si ulisema haujaniambia?”
“kukuambia kitu gani?”
“pale niliposema haunipendi, wewe ukasema haujaniambia kama haunipendi!”
“sasa je, kwani nilikuambia?
“kwa hiyo unanipenda?”
“ndio!”
“kivipi!”
“nafikiri tayari nilishakuambia kabla!”
“mimi Sitaki kama ulivyoniambia muda ule!”
“wewe unatakaje?”
“kimapenzi!”
“unasemaje?”
“nakupenda uwe mpenzi wangu!”
“Mpenzi wako?, yaani mimi na wewe tuwe katika mahusiano ya kimapenzi?”
“ndio!”
“usinifurahishe bwana, enhe ni kwa kipindi gani?”
“kipindi chote tu!”
“shida yako unifanye mimi mdoli wa kunichezea, sio?”
“hapana, sina nia hiyo kabisa!”
“kama hauna nia hiyo, sasa hivi tukirudi katika dunia yetu utawezaje kuniona mimi, hebu acha kuchekesha watu bwana!”
“dah!”
“dah kitu gani?”
“kwa hiyo haiwezekani?”
“haiwezekani na inawezekana pia!”
“kwa nini isiwezekane na iwezekane kwa pamoja?”
“haiwezekani kwa sababu Sitaki kuwa na mahusiano na wewe, sihitaji kuchezewa kabisa!”
“duh, enhe!”
“inawezekana kwa sababu mimi ni mwanamke!”
“sijakuelewa kabisa, nieleweshe basi!”
“hebu tuondoke hapa, twende tukakae na wenzetu wanaweza wakatufikiria vibaya!”
“kutufikiria vibaya, kwani kuna mtoto mdogo hapa kati yangu na wewe?”
“hakuna, ila haipendezi, kuwaacha peke yao harafu sisi tunajitenga huku, kama yule mzee akirudi asije kupata tabu tena ya kuanza kututafuta, kwanza alisema tusitoke pale!”
“sawa, wewe ndiye umeshinda, twende!” nilimuambia toka pale katika jiwe na taratibu tukaanza kurejea kule ambako mzee alituacha na kutuambia tusitoke.
“Aziza!”
“ndio!”
“hivi jina lako la kweli ni nani?” nilimuuliza
Itaendelea…

Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget