JINA LA HADITHI – KAZI YA SHETANI
SEHEMU YA -TATU
MWANDISHI - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com
SEHEMU YA -TATU
MWANDISHI - ASLAM KHAN
aslamstorymail@gmail.com
aslamstori.blogspot.com
Iliposhia…
“kiongozi wetu, sisi huwa hatukupingi mara nyingi kwani maamuzi ambayo huwa unayachukua huwa na matokeo mazuri baadae, ila swali langu ni kiumbe gani huyo ambaye umefikiria kumleta ili kutusaidia katika suala letu la kuirudisha nchi kule ilikotoka kwenye asili yetu watu wa Kopsheng?” mshirika mwengine aliuliza.
”Binadam, binadam ndio viumbe ambao nimefikiria kuwaleta ili kutusaidia kukabiliana na matatizo yanayotukabili” kiongozi alibainisha.
“binadam?!.....” aliuliza mmoja wao kwa mshangao akaendelea.

Endelea…
“hawa si ndo wale wanaokuja huku kila siku kuomba msaada na kwa tamaa yao ya kuwa maarufu, ukubwa wa cheo kazini au kupata mali si ndo wanawatoa wenzao kafara kwa ajili ya kupata damu?”
“sio kwamba samaki akioza mmoja wote watakuwa wameoza, hapana!...” alijibu kiongozi na kumeza funda kubwa la mate na kisha akaendelea
“endapo utakuwa unatupa samaki wote kwenye jalala baada ya mmoja wao kuoza, jua utakuwa unakosa mambo mazuri na muhimu katika maisha. Jaribu kuchambua na wapo wazima kati yao. Mara nyingi kiumbe kinachofanya mambo ya hovyo na uasi huitwa shetani, sasa hao mashetani wapo kwa binadam na hata kwetu pia. Leo tumekutana ili kujadili jinsi ya kuichukua nchi yetu toka kwa huyu shetani. Basi jua kua katika kundi la mambo, wengine ni kenge, nafikiri mtakuwa mmenielewa?”
“nndiooo…..hhapanan..!” kila mshiriki alijibu kwa jibu lake.
“Sijajua nini ambacho hakijaeleweka, ila tusipoteze muda kwa kuanza kuulizana maswali mmoja mmoja acha mimi nirejee kufafanua. Namaanisha kuwa sio kama binadam wote ni wenye tamaa sio woteni wenye tabia mbaya, la hasha!, wapo ambao wana tabia nzuri, wapo wenye hekima pia. Kwa hiyo kuhusu suala hilo msijali kabisa, tumeelewana hapo?” aliuliza tena kiongozi.
“ndiooooo!” washirika wote walijibu kwa kifupi.
“sawa..sawa..sawa, sasa tatizo lililopo ni kuwa, nilipanga waje binadamu wanne ili kuleta msaada, badala yake wapo watano. Kwa hiyo inaonyesha mmoja kati yao atakuwa hayupo katika mpango wetu, atakkuwa amepandikizwa. Sasa sijajua nani atakayekuwa amemleta na pia ameletwa kwa wema au kwa ubaya. Pia hata kumfahamu binadamu mwenyewe kwangu imekuwa ni vigumu, kwa hiyo hata silaha ile sijui ni nani wa kumpatia kwa sababu nahisi mmoja kati yao atakuwa ni binadamu mbaya” alimaliza
“kwa hiyo tunafanyaje kiongozi” mmoja wa washirika aliuliza. Wote walikaa kimya bila ya kujibu chochote wakionekana mawazo mazito kutawala vichwa vyao. Baada ya kimya cha takribani dakika tatu, mmoja wa washiriki alijikohoza kidogo hali iliyofanya wote waliokuwepo pale kugeuka na kumuangalia.
“aaaaah mimi naweza kuwatambua baadhi yao ila sio wote. Kwa wale waliokusudiwa, nitaweza kuwatambua wawili ama watatu tu, na hao mmoja wapo ndio atakayekuwa na hiyo silaha.” Alisema
“aaaah ila nimekumbuka, tatizo ni dogo sana kuhusu wa kumpa silaha, mnajua silaha hakuna atakayeweza kuichukua kama hatokuwa ni mtu sahihi.” Alisema.
“ni kweli, hilo wazo nilikuwa sina kabisa!” alisema kiongozi wao na kuendelea,
“kwa hiyo hapa kwa leo mkutano wetu umefungwa, mpaka pale tutakapoona kuna umuhimu wa kujulishana jambo jengine, basi tutajulishana.” Alisema kiongozi na kufunga kikao ambapo washirika wote walitawanyika na kuendelea na mambo mengine.
********************************************************************
Nilipata kuwaona watu ambao walikuwa ni binadamu kama nilivyo mimi.nilifarijika na kujiona ni mtu mwenye bahati ya kuwapata binadamu wenzangu ambapo niliamini kwa kiasi fulani wangeweza kunipatia msaada. Walikuwa ni watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili. Mwanaume mmoja alikuwa na asili ya kiarabu na mwengine alikuwa na asili ya kiafrika wakati mwanamke mmoja alikuwa shombe shombe wenye mchanganyiko wa kiarabu na kisomali na mwengine akiwa na asili ya kibantu. Nilivyowaangalia, walionekana ni watu waliokuwa wakielekezana jambo. Niliamua kusogea mpaka pale walipokuwepo.
“habari zenu ndugu zangu!” niliwasalimiaingawa sikuwa na uhakika kama kuna hata mmoja kati yao aliyeijibu salamu yangu. Wote waligeuka na kuniangalia.
“samahani ndugu zangu!” niliongea na kuendelea
“ninawaombeni msaada, jina langu ni Abdam. Kwa hali ambayo siifahamu nimejikuta tu nipo hapa. Sijajua ni kwa jinsi gani nimefika hapa. Nashindwa kujua hapa ni wapi na ni njia gani itakayonifanya niweze kurudi nyumbani salama”
“enhe kwa hiyo?” aliniuliza yule mmoja ya wanaume aliyekuwa na asili ya kiafrika zaidi.
“naombeni mnisaidie, ikiwezekana nipate kujua hapa nilipo ni wapi na kama mnaweza kunipatia msaada wa kurejea nyumbani!” niliwaambia. Hakuna aliyejibu, wote walikuwa wakiniangalia tu. Baada ya dakika takribani tatu hivi, mmoja kati yao aliongea
“Aziza unapajua hapa?”
“hapana!”alijibu kwa kifupi yule msichana mwenye asili ya mcanganyiko wa kiarabu na kisomali.
“Tina je?”aliendelea kuuliza.
“hapana!”
“Hamza?”
“hapana!”alijibu yule mwanaume mwenye asili ya kiarabu.
“sisi wote hatujui hapa tulipo ni wapi na pia tunashindwa ni kwa jinsi gani tunaweza kurejea nyumbani kwetu salama!” alisema yule mwanaume.
“kwa hiyo mnafanyaje?” niliuliza.
“kufanyaje? Kwani wewe unafanyaje, si kutafuta msaada au, mbona unauliza swali la kijinga hivyo, huo ni upumbavu” alijibu yule mwanaume.
“oh!” niliguna tu, kweli nilijiona nimeuliza swali ambalo lilikuwa ni la kipuuzi.
Wale watu waliendelea kusonga mbele, nami niliamua kuungana nao kwani hakukuwa na njia iliyo bora zaidi tofauti na kuandamana nao. Niliona ni bora kufuatana nao ili kutafuta msaada tukiwa tupo wengi tofauti na kama nikiwa nipo peke yangu. Hakuna aliyemsemesha mwenzake njiani. Tulitembea tukiwa katika hali hiyo ya kutosemeshana kwa takribani dakika arobaini hivi, ndipo kwa mbali tulipopata kumuona mzee mmoja aliyeonekana amesimama akiwa na fimbo yake.tofauti na watu wote tuliokutana nao njiani, huyu mzee sura yake ilikuwa inaonekana vizuri. Tulimsogelea yule mzee kwa minajiri ya kuomba msaada kwake. Alikuwa ni mzee mwenye nywele nyeupe kabisa. Wala haikuonekana nywele nyeusi kwake. Pia alikuwa amevaa yenye rangi nyeupe yaliyokuwa yanang’aa sana. Alishika fimbo ndefu iliyompita hata kimo chake kwa takribani sentimita mbili hivi. tuliamua kumsogelea yule mzee ambaye hakuwa akijali ujio wetu kwake.
“habari yako mzee?” tulimsalimia mara baada ya kumfikia pale alipokuwa amesimama hali iliyomfanya kustuka na kutuangalia. Hakujibu kitu bali aliishia kutuangalia tu.
“habari ya muda huu mzee?” tulimsalimia tena.
“salama, habari yenu?”
“nzuri mzee wetu!”
“vipi , mnataka niwasaidie nini mbona munaniangalia hivyo?”
“samahani mzee wetu!”
“enhe!”
“tunaomba msaada wako, tunaomba utusaidie!”
“msaada gani munaouhitaji tokea kwangu?”
“kama itawezekana tujue ni kwa jinsi gani tutaweza kurudi nyumbani!”
“msinishangaze bwana, kwani huko mlikotoka ni wapi?”
“hatujui!”
“kama hamjui mlikotoka, sasa hapa mlifikaje?”
“hatujui mzee wetu”
“wewe unaitwa nani?” aliuliza yule mzee huku akimuonyeshea kidole hamza.
“hamza”
“sawa, enhe ilikuwaje ukafika katika eneo hili?”
“sijui mzee wangu”
“haujui?, hebu elezea ilikuwaje ukawa katika sehemu hii, yaani tukio la mwasho kulikumbuka?”
“ahnha ni..ni...nili...nilikuwa natoka nyumbani ili kuelekea kwa rafiki yangu ghafla nikiwa njiani nikahisi kuishiwa nguvu harafu kuna upepo nikahisi ulikukwa unavuma sana. Ulikuwa ni upepo mkali sana hali iliyonifanya kufumba macho ili mchanga usije ukaingia machoni. Nilishindwa kukimbia kutokana na kuishiwa nguvu. Baada ya dakika kadhaa nguvu zilirudi na ule upepo ulikuwa umeisha. Nilipokuja kufungua macho, nilistaajabu kwa sababu sikuwepo pale, nilikuwa katika sehemu nyengine, sehemu yenye mazingira ambayo siyafahamu, ni mazingira haya katika sehemu hii!” alimaliza hamza. Ilikuwa ni hadithi ya kustaajabisha kidogo.

Kitaendelea kitu gani, usikose sehemu inayofuata
Post a Comment