Jina la hadithi. : SHANGAZI II
Sehemu ya : KUMI NA MOJA (11)
Mwandishi : Aslam Khan
mawasiliano : aslamstorymail@gmail.com
Ilipoishia...
Kutoka mpaka kufikia mbagala rangi tatu ilituchukua nusu saa nzima. Tulipofika mbagala, basi liliingia kituoni tena, nikiwa na mawazo mengi, nilistuka mara baada ya kusikia sauti nzuri na nyororo ikiniambia jambo. Sikuelewa anaongea kitu gani, hivyo ikanibidi niinue kichwa changu ili kumuangalia aliyekuwa ananiongelesha. Alikuwa msichana, mwenye weusi wa wastani akiwa anang'aa bara bara, wenyewe wanaitaga black beauty.
"Sogea kule dirishani, hii ni siti yangu!" Alisema
Endelea...
"Hapa nilipokaa ndio kwenye siti yako?"
"Ndio!"
"Hebu tiketi yako kwanza niione!"
"Hii hapa, si unaona siti namba ishirini na tano hii!"
"Mbona na ya kwangu imeandikwa hivyo hivyo!"
"Tutamuuliza konda, wewe sogea kule nipumzike!"
"Kwani unatoka mbali sana na umechoka?" Nilimuuliza lakini hakunijibu kitu chochote.
Kwa sababu hakunijibu kitu chochote, niliamua kusogea kule kwenye siti ya dirishani. Baada ya muda, basi lilianza kuondoka katika kituo cha Mbagala rangi tatu. Mwendo ulianza kwa kuwa mdogo hasa kutokana na foleni iliyokuwa inapatikana katika barabara ya Kilwa mpaka kufikia eneo la kongowe. Ilituchukua takribani dakika hamsini kutoka katika kituo cha mbagala rangi tatu mpaka kufika kongowe, eneo lililokuwa linatenganisha mkoa wa Dar es salaam na Pwani. Tuliendelea kwenda kwa mwendo wa wastani mpaka tulipofika katika eneo la mwandege, ambapo mwendo ulibadilika na kuwa mwendo wa kasi. Roho yangu ilikuwa ikiomba dua muda wote tufike salama, huku nikiyafaidisha macho yangu kwa kuangalia miti iliyokuwa inakimbizana kwa kurudi nyuma. Tulipofika ikwiriri, basi liliingia kwenye mizani na baada ya kutoka likaenda kuegesha mbele kidogo tukipewa fursa ya kununua chochote kwa dakika zisizozidi tano.
"Nichukulie hindi hapo!" Sauti ya yule binti iliniambia hali iliyonifanya nistuke kwa kujua alitaka nimnunulie mahindi kwa kutumia hela yangu. Ilibidi nimuangalie usoni ili nijue alikuwa anamaanisha kile alichokuwa anakiomngea au lah!.
"Shika hela hii, nichukulie mahindi ya mia tano!" Aliendelea kusema huku akiwa ananipatia hela aliyokuwa ameishika mkononi mwake. Niliichukua na kumpa muuzaji kisha akanipatia kile nilichokuwa nimekihitaji.
"Hili hapa!" Nilimpatia huku nikimuangalia usoni. Alipokea na kuanza kula taratibu. Nilijifanya kujikausha kimya bila ya kuongea nae nikisubiri kama angeweza kuanzisha mazungumzo.
Safari iliendelea mpaka kufika katika daraja la mkapa, la mto rufiji bila ya mtu yeyote kumsemesha mwenzake. Nilichungulia dirishani ili kuyaangalia mazingira mazuri na ya kuvutia yaliyopatikana katika eneo la daraja hili refu.
"Tupo Rufiji eeeh!" Aliuliza huku ajijaribu kuangalia nje kupitia pale dirishani.
"Ndio, darajani!" Nilijibu huku kwenye moyo wangu nikiwaza kuwa huo ndio ulikuwa wakati sahihi wa kuanzisha mazungumzo.
"Oooh..!"
"Vipi, unaenda wapi wewe?" Nilianza kumuuliza swali huku nikimuangalia usoni, hasa mdomo wake uliojazana na nyama za kutosha.
"Mtwara..!"
"Ooh hata mimi naelekea huko huko, vipi unapajua vizuri!"
"Kivipi, kama kupajua, napajua!"
"Wewe ni mwenyeji wa huko!"
"Kwa kiasi fulani naweza kusema hivyo, ingawa sio mwenyeji sana!"
"Kwa nini?"
"Huku naenda kwa baba mdogo, kutembea tu, ila mara kwa mara huwa nakuja huku kwa hiyo inawezekana kuwa mwenyeji kwa kiasi fulani"
"Aha, na unafikia sehemu gani?"
"Shangani, sijui wewe unafikia wapi?"
"Aah hata sipajui!"
"Hahaha kumbe ni mgeni kabisa, unavyouliza utafikiri kama ni mwenyeji vile, kumbe ni mgeni!"
"Aaah ila nashukuru nimekupata mwenyeji, unaweza kuwa mwenyeji wangu!"
"Nani, mie? Haya!"
"Unaweza kunifahamisha jina lako?"
"Naitwa Tunda!"
"Aaah dah nakumbuka mziki wa muumin mwinjuma nikilisikia jina lako!"
"Mziki gani huo?"
"Unaitwa Tunda kama lilivyojina lako!"
"Huo mziki ni wa zamani eeeh maana mie siujui mziki unaoitwa hivyo!"
"Ndio, zamani sana kabla ya wewe kuzaliwa!"
"Unaonekana mcheshi sana, unaweza kuniimbia kidogo labda kama naufahamu!"
"Sauti yangu mbaya, harafu itakuwa kero kwa abilia wengine, labda...!"
"Labda nini?"
"Labda nikuandikie mashairi yake kwenye meseji!"
"Haya nitumie!"
"Nakutumiaje na namba yako sina jamani!"
"Kumbe ndo unaomba namba kijanja, sio?"
"Hapana bwana, si nakutumia mashairi tu, harafu nakupa simu yangu unaifuta namba yangu!"
"Aha, hapo sawa, andika, sufuri.......tisa....saba....mbili!"
"Sawa, naweza kuisave!"
"Usiihifadhi, si unanitumia mara moja tu kisha unaifuta, usisave bhana!"
"Sawa, ngoja nikuandikie!" Nilimjibu huku nikianza kuandika mashairi ya wimbo wa tunda wa muumin mwinjuma.
"JAMANI TUNDA, NITALIPATAJE TUNDA... TUNDA TAMU TAMU!" Niliandika na kumtumia.
"Mmmmh!" Nilimsikia akiguna, nilimtazama nae alikuwa alitabasamu tu na kuendelea akakuiinamia kwenye simu yake. Wakati nikiendelea kutafakari, simu yangu ilitoa mlio kuashiria kuna meseji ilikuwa imeingia. Nilifungua na kusoma.
"KWANI NDO IMEISHIA HAPA, ENDELEA BHANA NIMEPENDA!" Ilikuwa ni meseji kutoka kwa Tunda. Nilimuangalia Tunda ambaye alikuwa anatabasamu tu muda wote. Nilianza kujiuliza na kuona hayo mashairi ya mbele nilikuwa ninaelekea kudanganya. Niliwaza ili hata kama kudanganya, nisidanganye sana.
"NILIPOKUWA MDOGO MWENZENU MIMI, NILIKUWA SIJUI NINI MAANA YA MAPENZI, NA HIVI SASA NIMESHAKUWA, NAELEWA NINI KITU KUPENDA, BABY BABY NALIA MIMI, BABY BABY NAHUZUNIKA, NIKIKOSA KUKUONA KWA MUDA WA SIKU MOJA TU, SINA RAHA MWENZAKO, OOH OOH BABY, NAKUPENDA. SI WA KWANZA MIMI KULILIA LAKO PENZI, TOKA ENZI ZILE ZA MABABU ZETU X2, JAMANI BABY NAMPENDA KULIKONI WOTE...!" Niliiandika na kuituma.
"ENDELEA!"
"AAAH JAMANI, NYIMBO YENYEWE NDEFU SANA!"
"HARAFU UMETUNGA NA MASHAIRI YAKO, SIO HAYA!"
Nilipoisoma ile meseji, nilishindwa hata kujibu kitu
"Vipi, mbona kimya?" Tunda aliniuliza kwa mdomo mara baada ya kuona sijatuma meseji kwa muda mrefu.
"Hamna kitu, unataka tuwe tunachat?"
"Wewe tu, sio mbaya!"
"Sawa!" Nilijibu huku nikifikiria neno la kuanza nalo. Nilitafakari kwa muda, mara simu yangu ikatoa sauti tena.
"NIAMBIE, MBONA KIMYA!" Meseji kutoka kwa Tunda ilisomeka.
"TUNDA...!"
"ABEE!"
"WEWE NI MZURI SANA!" Nilimtumia meseji iliyomfanya Tunda kuguna.
"Wewe!" Nilisikia maneno yakiwa yamemtoka Tunda. Nilianza kuwa na wasi wasi.
"HIVI NIKUULIZE?" Tunda alinitumia meseji hiyo...
Kipi anachotaka kuuliza?
Usikose sehemu inayofuata...
Post a Comment